Wednesday, August 30, 2023

Active Mama anavyookoa soko la nazi mkoa wa pwani

 

WAKINAMAMA  mbalimbali kutoka mkoa wa pwani wamesema wamekuwa wakinufaika na kilimo cha nazi baada ya wawekezaji wengi kuwekeza katika bidhaa ya nazi na kufanya  kilimo hicho  kupanda thamani.

Akizungumza na mwandishi , mfanyabiashara wa kuuza na kubangua nazi, Khadija Mohamed amesema zao hilo limekuwa likipata umaarufu mkubwa kutokana na watu wengi kutumia mafuta ya nasi katika kujipakaa.

Alisema anamshukuru sana mkurugenzi wa Active Mama, Ernestina Mwenda ‘Cocunut Lady’ kutokana na kuwaunga mkono kwa kununua nazi nyingi  ambazo zinawasaidia katika kujikimu katika maisha yao ya kila siku.

 

Alisema kampuni ya Active Mama imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasaidia wakinamama wengi kwa kununua nazi katika maeneo yao na kufanya ubanguaji wa nazi hali ambayo inafanya inawapa ajira mara mbili.

“Kwanza tunauza nazi ambapo tumekuwa tukipata fedha za kutosha, lakini pia amekuwa akibangua nazi na kufanya tupate ajira nyingine” alisema Khadija.

Ernestina  alisema amekuwa akitumia nazi za asili katika kutengeneza mafuta ya Active Mama, ikiwa kama sehemu ya kuunga mkono kilimo cha nazi lakini pia kuifanya jamii kutotumia kemikali katika miili yao.

“Unapotumia mafuta ya nazi ya asili, unafanya ngozi yako ibaki katika ubora unaostahili, lakini pia unasaidia kilimo cha nazi kwa ndani ya nchi.

Mwisho

 

Friday, July 14, 2023

Rais Dr Mwinyi amuaga balozi wa Uturuki


 *RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amemtaka Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uturuki Mhe.Idd Seif Bakari kuendeleza   uhusiano uliopo , kudumisha diplomasia ya kiuchumi , kusaidia  kutafuta fursa mbalimbali za uwekezaji pamoja na  biashara zipatikanazo katika nchi ya Uturuki. 


Ameyasema hayo leo alipokutana na Balozi Idd Seif Bakari aliyefika Ikulu Zanzibar  kumuaga kuelekea katika kituo chake cha uwakilishi nchini Uturuki baada ya uteuzi wake hivi karibuni. 




Aidha, Rais Dk Mwinyi amegusia mambo matatu katika kufungua fursa za uwekezaji na biashara kati ya Zanzibar na Uturuki ikiwemo kupata  wawekezaji katika viwanda kwa maendeleo  waliyopiga kupitia sekta hiyo kuja kuwekeza nchini, eneo la pili   kuzitangaza fursa  zilizopo katika sekta ya utalii  wa fukwe za bahari na urithi  pia kupitia kuwepo kwa  usafiri wa ndege ya shirika la Uturuki linalofanya safari zake za moja kwa moja hapa nchini kutangaza vivutio  vinavyopatikana nchini, eneo la tatu kujifunza na kutafuta fursa za uwekezaji zitokanazo na sekta ya miundombinu ikiwemo bandari, barabara, na viwanja vya ndege.

Balozi Idd Seif Bakari aliteuliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Aprili 05 Mwaka huu, kabla ya uteuzi huo alikuwa Konseli Mkuu, Dubai.


Rais Samia kuwa mwenyeji Mkutano wa Wakuu wa nchi Afrika


Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu utakaofanyika  jijini Dar-es-salaam kuanzia tarehe 25 mpaka 26 Julai 2023 katika Ukumbi wa JNCC.


Lengo la Mkutano huo  ni majadiliano ya Wakuu wa nchi za Afrika katika kutatua changamoto mbalimbali za ukuaji wa uchumi Afrika kupitia rasilimali watu.

Mkutano huo utajadili uwekezaji kwenye Rasimali watu ili kuongeza tija na ajira kwa vijana, kushughulikia maendeleo ya ukuaji wa Sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Nishati na Miundombinu kama  kichocheo katika kukuza uchumi na kuondoa umasikini.

Ni matarajio yetu kutakuwa na fursa nyingi kwa sekta binafsi Tanzania na kwa nawajasiriamali ambao watafaidika na wageni watakaokuja kwenye mkutano huo kwa kufata fursa ya kuuza bidhaa zao na kutoa huduma mbalimbali.

Wednesday, October 26, 2022

Basata kutoa vyeti kwa wanafunzi kupitia UNI AWARD

 


Baraza  la Sanaa la Taifa ‘BASATA’ pamoja waanzilishi wa tamasha la kutafuta vipaji vyuoni ‘UNI AWARD’ , wanatarajia kuanza kwa msimu wa wanne wa watamasha hilo litakalokutanisha zaidi ya vyuo 29 nchi nzima.

Akizungumza katibu mtendaji wa Basata , Kedmon Mapana alisema Serikali baada ya kuona jitihada ya vijana hao kwa zaidi ya misimu mitatu, waliamua kuwaunga mkono kwa kuwasaidia kufika mbali  kwa kuungana nao.


 

Alisema Basata tayari imeongea na idara zingine za Elimu katika kuhakikisha wanatoa  vyeti kwa wanafunzi  wa tuzo mbalimbali,  katika kutambua mchango wa masomo ya Sanaa katika vyuo.

 “Washindi zaidi ya kupewa tuzo na cheti, lakini pia wataweza kuwa miongoni mwa wanufaika wa mikopo ya sanaa inayoenda kuzinduliwa hivi karibuni na hapa kuendelezwa katika chuo cha Sanaa Bagamoyo” alisema.

Alisema Serikali bado inaandaa mazingira kwaajili ya kuhakikisha watu wenye vipaji wanajiajiri lakini pia wanawezeshwa .


 

Mkurugenzi wa Uni Award  Joseph Ndalo, alisema wanatarajia kwenda katika vyo mbalimbali, lakini pia safari hii watafika hadi Zanzibar katika kuhakikisha kwamba wanawafikia wanafunzi wote.

“Tunashukuru kwa Serikali kutuunga mkono baada ya kutafuta washiriki, watakaa kambi siku tano na baada ya hapo tutafanya tamasha la mwisho hapa Dar es Salaam” alisema.

 

Tuesday, October 25, 2022

Tanesco -Saccos waungana na Tanesco Ltd katika ushirikiano bora


 

MKURUGENZI wa Rasilimali watu na Utawala wa Shirika la Umeme Tanzania ‘TANESCO’  Francis Sanguna amesema wamefanikiwa kusaini muswada wa kuwaunganisha  Tanesco Saccos na Tanesco Ltd  ili  kujenga mifumo imara na endelevu wa ukusanyaji akiba, hisa na amana.

Akizungumza na  jana wakati wa mkutano mkuu na  wanachama wa Chama cha Ushirika na Kukopa ‘Tanesco Saccos’  Sanguna alisema  duniani kote vyama vya ushirika na kukopa ni nguzo muhimu, na vimekuwa vinachangia ukuaji wa uchumi na  pato la taifa.

Alisema kati ya wafanyakazi 7000 wenye mikataba ya kudumua wafanyakazi 6000 ni wanavchama wa Ushirika huo, ambapo wanaendelea kuwashauri  na  wafanyakazi wapya   kujiunga.

"Vyama hivi vimekuwa na mchango mkubwa sana  ni nguzo ya uchumi wa nchi bodi ya Tanesco,  inatambua umuhimu huo na kutaka  uongozi wa Saccoss kutekeleza malengo yake  na kusimamia yale waliyojiwekea.

Wanachama waendelee kuchangia katika chama pamoja na kutumia mifuko ya Tehama ikiwemo huduma ya kiganjani kupitia simu," alisema

Mwenyekiti wa Chama cha Tanesco Saccos Somoe Nguhwe amesema pamoja na kutoa mikopo kwa wanachama, wamekuwa na utaratibu wa kujali  jamii kwa kutoa msaada.

  "Mkutano mkuu wa mwaka huu tunaangalia mapato na matumizi ili mwaka  2022 tujue tufanye nini, lakini pia  tunaendelea kuwa karibu na jamii kwa kwenda kutoa mashuka katika hospitali ya kansa  Ocean Road," alisema.


Katika mkutano  huo  wanachama waliweza kupatiwa tuzo na mgeni rasmi katika upande wa mwanachama bora katika uwekaji akiba, mwanachama bora upande wa mikopo na mwanachama bora  kwa upande  matumizi ya Tehama.

Naye mwanachama na mfanyakazi wa Tanesco Monica Masawe amesema chama hicho kimeweza kumsaidia kupata  mkopo wa elimu wakati anahitaji kujiendeleza, pia amesomesha watoto wake pamoja na kujipatia fedha za kuanzisha miradi midogo midogo ya ufugaji wa Kuku wa mayai.

mwisho

Agri Thamani wawapa thamni mama Ntilie kwenye tamasha la Msosi Asili

Taasisi ya Agri Thamani  ikishrikiana na Umoja wa Ulaya (EU) imewataka jamii kuwa na utamaduni wa kula  vyakula vya asili, ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama Corona na kuboresha afya ya mwili

Akizungumza katika uzinduzi wa Tamasha la 'Msosi Asili' mkurugenzi wa Taasisi ya Agri Thamani  na  Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Mashirika yasiyo ya Kiserikali(NGos) Neema Lugangira alisema vyakula vya asili vina virutubisho kinga mwili ambapo vinatusaidia kujikinga na maradhi ya mlipuko ndiyo maana tulikuwa tukitumia vyakula vya asili katika kujikinga na  corona.

anasema matamasha hayo yatakuwa yakifanyika mikoa mbalimbali, katika kuwapa watu elimu kwaajili ya kutumia vyakula vya asili kwakuwa nchi zilizoendelea vyakula hivyo vinauzwa kwa ghalam kubwa wakati nchi za Afrika hasa Tanzania ndo vinauzwa kwa ghalama ndogo lakini bado watu hawapendi kula.


 Mgeni rasmi katika maonesho hayo, Mariam Mtesa ambaye ni mwenye kiti wa Mama Lishe na Baba Lishe wilaya ya Temeke,  anasema anashukuru kwa taasisi ya Agri Thamani, wakishirikiana na Wizara ya Kilimo,  Shirika la Chakula Duniani 'FAO' na Umoja wa Ulaya 'EU' kwa kuwajali mama lishe wa mtaani kwa kuwapa semina na kuwaandalia maonesho.


Anasema wafanyabiashara wa chakula mama lishe na baba lishe, wamekuwa wakipitia wakati mgumu hasa katika mazingira ambapo wamekuwa wakihamishwa hamishwa huku na kule bila ya kuwa na mpangilio maalum.

Mtesa anasema kupitia matamasha kama hayo na kuwapa nafasi kuwa kama mgeni rasmi, inaonesha wazi kwamba wamewajali, kwakuwa wao wanakuwa wakihudumia watu wengi sana kwa wakati mmoja.

 Mwakilishi wa Balozi wa EU,Anna Constine,alisema EU itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania kuhakikisha jamii zinatumia vyakula vya asili kwaajili ya kujenga afya.


mwakilishi wa FAO Charles Tulahi alisema wataendelea kuhamasisha ulaji wa vyakula vya asili kwasabu vinaleta nguvu zaidi ukilinganisha na vyakula vingine vya kisasa.

Naye Afisa Kilimo Mkúu kutoka Wizara ya Kilimo,Magreth Natai alisema,serikali inaendelea kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula(FAO) kuhakikisha Watanzania wanaachana na ulaji wa vyakula visivyofaa na kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza.