Friday, July 14, 2023

Rais Samia kuwa mwenyeji Mkutano wa Wakuu wa nchi Afrika


Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu utakaofanyika  jijini Dar-es-salaam kuanzia tarehe 25 mpaka 26 Julai 2023 katika Ukumbi wa JNCC.


Lengo la Mkutano huo  ni majadiliano ya Wakuu wa nchi za Afrika katika kutatua changamoto mbalimbali za ukuaji wa uchumi Afrika kupitia rasilimali watu.

Mkutano huo utajadili uwekezaji kwenye Rasimali watu ili kuongeza tija na ajira kwa vijana, kushughulikia maendeleo ya ukuaji wa Sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Nishati na Miundombinu kama  kichocheo katika kukuza uchumi na kuondoa umasikini.

Ni matarajio yetu kutakuwa na fursa nyingi kwa sekta binafsi Tanzania na kwa nawajasiriamali ambao watafaidika na wageni watakaokuja kwenye mkutano huo kwa kufata fursa ya kuuza bidhaa zao na kutoa huduma mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi