Friday, July 14, 2023

Rais Dr Mwinyi amuaga balozi wa Uturuki


 *RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amemtaka Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uturuki Mhe.Idd Seif Bakari kuendeleza   uhusiano uliopo , kudumisha diplomasia ya kiuchumi , kusaidia  kutafuta fursa mbalimbali za uwekezaji pamoja na  biashara zipatikanazo katika nchi ya Uturuki. 


Ameyasema hayo leo alipokutana na Balozi Idd Seif Bakari aliyefika Ikulu Zanzibar  kumuaga kuelekea katika kituo chake cha uwakilishi nchini Uturuki baada ya uteuzi wake hivi karibuni. 




Aidha, Rais Dk Mwinyi amegusia mambo matatu katika kufungua fursa za uwekezaji na biashara kati ya Zanzibar na Uturuki ikiwemo kupata  wawekezaji katika viwanda kwa maendeleo  waliyopiga kupitia sekta hiyo kuja kuwekeza nchini, eneo la pili   kuzitangaza fursa  zilizopo katika sekta ya utalii  wa fukwe za bahari na urithi  pia kupitia kuwepo kwa  usafiri wa ndege ya shirika la Uturuki linalofanya safari zake za moja kwa moja hapa nchini kutangaza vivutio  vinavyopatikana nchini, eneo la tatu kujifunza na kutafuta fursa za uwekezaji zitokanazo na sekta ya miundombinu ikiwemo bandari, barabara, na viwanja vya ndege.

Balozi Idd Seif Bakari aliteuliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Aprili 05 Mwaka huu, kabla ya uteuzi huo alikuwa Konseli Mkuu, Dubai.


No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi