Taasisi ya Agri Thamani ikishrikiana na Umoja wa Ulaya (EU) imewataka jamii kuwa na utamaduni wa kula vyakula vya asili, ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama Corona na kuboresha afya ya mwili
Akizungumza katika uzinduzi wa Tamasha la 'Msosi Asili' mkurugenzi wa Taasisi ya Agri Thamani na
Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Mashirika yasiyo ya
Kiserikali(NGos) Neema Lugangira alisema vyakula vya asili vina virutubisho kinga mwili ambapo vinatusaidia kujikinga na maradhi ya mlipuko ndiyo maana tulikuwa tukitumia vyakula vya asili katika kujikinga na corona.
anasema matamasha hayo yatakuwa yakifanyika mikoa mbalimbali, katika kuwapa watu elimu kwaajili ya kutumia vyakula vya asili kwakuwa nchi zilizoendelea vyakula hivyo vinauzwa kwa ghalam kubwa wakati nchi za Afrika hasa Tanzania ndo vinauzwa kwa ghalama ndogo lakini bado watu hawapendi kula.
Mgeni rasmi katika maonesho hayo, Mariam Mtesa ambaye ni mwenye kiti wa Mama Lishe na Baba Lishe wilaya ya Temeke, anasema anashukuru kwa taasisi ya Agri Thamani, wakishirikiana na Wizara ya Kilimo, Shirika la Chakula Duniani 'FAO' na Umoja wa Ulaya 'EU' kwa kuwajali mama lishe wa mtaani kwa kuwapa semina na kuwaandalia maonesho.
Anasema wafanyabiashara wa chakula mama lishe na baba lishe, wamekuwa wakipitia wakati mgumu hasa katika mazingira ambapo wamekuwa wakihamishwa hamishwa huku na kule bila ya kuwa na mpangilio maalum.
Mtesa anasema kupitia matamasha kama hayo na kuwapa nafasi kuwa kama mgeni rasmi, inaonesha wazi kwamba wamewajali, kwakuwa wao wanakuwa wakihudumia watu wengi sana kwa wakati mmoja.
Mwakilishi wa Balozi wa EU,Anna Constine,alisema EU itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania kuhakikisha jamii zinatumia vyakula vya asili kwaajili ya kujenga afya.
mwakilishi wa FAO Charles Tulahi alisema wataendelea kuhamasisha ulaji wa vyakula vya asili kwasabu vinaleta nguvu zaidi ukilinganisha na vyakula vingine vya kisasa.
Naye Afisa Kilimo Mkúu kutoka Wizara ya Kilimo,Magreth Natai alisema,serikali inaendelea kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula(FAO) kuhakikisha Watanzania wanaachana na ulaji wa vyakula visivyofaa na kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi