Baraza la Sanaa la Taifa ‘BASATA’ pamoja waanzilishi wa tamasha la kutafuta vipaji vyuoni ‘UNI AWARD’ , wanatarajia kuanza kwa msimu wa wanne wa watamasha hilo litakalokutanisha zaidi ya vyuo 29 nchi nzima.
Akizungumza katibu mtendaji wa Basata , Kedmon Mapana alisema Serikali baada ya kuona jitihada ya vijana hao kwa zaidi ya misimu mitatu, waliamua kuwaunga mkono kwa kuwasaidia kufika mbali kwa kuungana nao.
Alisema Basata tayari imeongea na idara zingine za Elimu katika kuhakikisha wanatoa vyeti kwa wanafunzi wa tuzo mbalimbali, katika kutambua mchango wa masomo ya Sanaa katika vyuo.
“Washindi zaidi ya kupewa tuzo na cheti, lakini pia wataweza kuwa miongoni mwa wanufaika wa mikopo ya sanaa inayoenda kuzinduliwa hivi karibuni na hapa kuendelezwa katika chuo cha Sanaa Bagamoyo” alisema.
Alisema Serikali bado inaandaa mazingira kwaajili ya kuhakikisha watu wenye vipaji wanajiajiri lakini pia wanawezeshwa .
Mkurugenzi wa Uni Award Joseph Ndalo, alisema wanatarajia kwenda katika vyo mbalimbali, lakini pia safari hii watafika hadi Zanzibar katika kuhakikisha kwamba wanawafikia wanafunzi wote.
“Tunashukuru kwa Serikali kutuunga mkono baada ya kutafuta washiriki, watakaa kambi siku tano na baada ya hapo tutafanya tamasha la mwisho hapa Dar es Salaam” alisema.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi