Naibu Waziri wa Ujenzi Atupele Mwakibete amezindua Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi na kutoa maagizo manne ikiwa kushughukia sheria ya Majenzi,Mwongoza Kanuni na kuipa heshima tasnia hiyo
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mwakibete alisema mataifa mengi yamekuwa yakiendelea kutokana na bodi kama hizo kwakuwa wamepewa dhamana kubwa ya kusimamia Baraza la Taifa la Ujenzi 'NCC na kuratibu maendeleo ya sekta ya ujenzi nchini
Mwakibete alisema taasisi ya NCC iliundwa ili kuishauri Serikali na kutoa ushauri kwa wadau wa ujenzi kwakuwa ina mchango mkubwa katika kujenga miundo mbinu hapa nchini
Alisema hata hivyo hadi sasa kutokana na changamoto mbalimbali jukumu hilo la NCC halijatekelezwa ambapo pia walikuwa na kazi ya kuandaa miongozo ya gharama ya ujenzi, kuratibu utekerezaji wa sera ya ujenzi na kuwa sekretalieti ya kamati ya kuratibu utekerezaji wa sera ya ujenzi.
Tunajua NCC imekuwa haipati fedha za maendeleo hata vyanzo vyenu vya mapato vinategemea sana kutokana na gharama ya ushauri wa wadau na kusimamia migogoro inayotokana na wadau wa ujenzi
Vyanzo hivyo vya fedha havijitosherezi wala bajeti yake haitabiriki kwa hiyo bodi mnajukumu la kuwa na vyanzo vya mapato vya kuendesha taasisi" alisema
Alimalizia kwa kuwataka kusiwe na upendeleo katika migogoro ambayo imekuwa ijitokezą kama mtu ataona yupo kwenye mgogoro huo unamuhusu ni bora kumpisha mwanabodi mwingine kufanya maamuzi lakini sio yeye kwakuwa wataanza kutia mashaka mwisho alitaka bodi kushughulikia ongezeko la fedha ambalo limekuwa likizidi maradufu kutokana na bajeti ya awali ya ujenzi.
Mwenyekiti wa bodi hiyo Dr Fatma Mohamed, alipokea vitendea kazi kutoka kwa naibu Waziri huyo na kusema watayatendea kazi yale yote ambayo wameambiwa.
mwisho
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi