Wednesday, September 14, 2022

Mutta asaidia watu wenye Saratani kupitia taasisi ya Dr Getrude Rwakatare


 DIWANI wa kata ya Kawe Mutta Rwakatare anatarajia kutembelea wagonjwa wa kansa na kuwasaidia matiti ya banndia katika hospitali ya Ocean Road ikiwemo  kuzindua taasisi ya Dr Getrude Rwakatare itakayosaidia watu wenye magonjwa na matatizo mbalimbali.

alisema taasisi hiyo itazinduliwa  8 Oktoba mwaka huu, ikiwa na  lengo ya kuyaendelea yale mazuri aliyokuwa akiyafanya mchungaji kiongozi  wa  Kanisa la Mlima wa Moto na aliyekuwa mbunge wa viti maalum Getrude Rwakatare.

Rwakatare alisema lengo la  kutembeleaa wagonjwa wenye saratani na kuwasaidia matiti ya bandia kunatokana na wanawake wengi wanaokatwa matiti wanakosa kujiamini, hivyo wanapopata yale  ya bandia kidogo yanawaongezea kujiamini.

 “Tunaomba taasisi zingine ambazo zinaweza kujitokeza kwenye matembezi ambayo tutaanzia kwenye hoteli ya Serena  kuelekea kwenye hospitali  hiyo.

Lakini pia tunaruhusu watu kuleta vitu mbalimbali kwaajili ya kuwasaidia wagonjwa wa Saratani, ambao vinawasilishwa moja kwa moja kwa mgonjwa” alisema.

Alisema zaidi ya matiti ya bandia ambapo kila moja linauzwa kwa zaidi ya Sh 150,000  ameomba watu pia kujitokeza kwaajili ya kuchangia kile ambacho wanakiweza ambavyoo anafikishiwa mgonjwa moja kwa moja.

Aliongeza kwa kusema lengo la taasisi hiyo ni kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali, lakini wameanza na kansa sababu Oktoba ni mwezi wa maadhimisho ya kansa duniani.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi