MTANDAO wa Wanawake Watetezi waHaki za Binaadam Tanzania (CWHRDT) wamezindua dira ya miaka mitano yenye lengo la kuwatetea watetezi wanawake ili wafanyekazi katika mazingira salama.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, mratibu wa mtandao wa CWHRDT Hilda Dadu alisema dira hiyo itasaidia katika kulinda usalama wa watetezi wa wanawake katika jamii dhidi ya vitisho vinavyotolewa kwao.
Alisema wanazo zaidi ya kesi tano za vitisho walizofanyiwa watetezi wa wanawake, ambao walidiriki kuwatetea wanawake waliokuwa wakitaka kubakwa, kufanyiwa ukeketaji na ulawiti kutoka katika jamii za watu ambao ndugu zao walikuwa wakituhumiwa.
Lengo la kufanya hivyo ni kutaka watetezi hao kuachana na kesi hizo ili kuwarudisha nyuma katika harakati zao za utetezi wa wanawake jambo ambalo limekuwa likiwafanya kukata tamaa.
“Watetezi wengi wamekuwa wakirudi nyuma na wengine kuacha kabisa, baadaya ya vitisho hivyo kutoka kwa jamii wakiamini ndugu zao wataenda jela”
Alisema pia dira hiyo itakuwa ikiwapa muongozo baada ya kufanya kazi kwa kufuata matukio badala yake watakuwa wakifanya kazi kwa kufuata muongozo waliojipangia.
“Maombi yetu kwa wadau na Serikali tufanye kazi kwa pamoja ili kuimarisha hali ya ulinzi na usalama, ili wanawake watetezi wa haki za wanawake wafanye kazi katika hali ya usalama” alisema.
Dadu pia aliiomba jamii iache kuwapa majina mabaya watetezi hao wa wanawake, ambayo mara nyingi yamekuwa kama udhalilisha kwa kuwaita majina ua wavunja ndoa, Malaya na majina mengine ambayo hayana Maadili.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi