Wednesday, April 13, 2022

COSOTA waingia mkataba na Suma JKT kukusanya mirabaha


 

TAASISI ya Haki Miliki Tanzania (COSOTA) imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya SUMA JKT Auction Mart Ltd kwaajili ya kukusanya mirabaha ya wasanii wa muziki Tanzania.

Akizungumza katika utiaji wa saini  leo katika ofisi za Cosota jijini Dar es Salaam, kaimu Afisa mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakiliki Philimon Kilaka anasema mkataba huo ni kwaajiliya kukusanya fedha katika sehemu zote wanazotumia kazi za sanaa za muziki.

Anasema miongoni mwa sehemu ambazo wanatarajia Suma Jkt watakuwa wakipita kuchukua fedha za mirabaha ambazo zinatokana na utumiaji wa nyimbo za wasanii ni kwenye mabaa, Hoteli, kwenye vituo vya redio na sehemu zingine ambazo zipo kwa mujibu wa sheria.

Kilaka  anasema mkabata huo utahusisha katika mikoa miwili, ambapo ni Dodoma na Dar es Salaam, huku mkoa wa Arusha ttayari yupo wakala mwingine ambapo anahusika na ukusanyaji wa mirabaha hiyo wakati mikoa mingine ya Tanzania Cosota wanashirikiana na wadau wengine katika ukusanyi wa mirabaha hiyo.

 


 

“Hawatatumia nguvu kwakuwa jambo hili lipo kisheria na wala hatutegemei mtu kufunga sehemu yake ya biashara kwaajili ya kuwakimbia watu ambao wanakusanya mirabaha hiyo” alisema.

Mwakilishi wa mkurugenzi mwendeshaji na mkurugenzi wa huduma za kisheria , Meja Jamal  Mohamed alisema taasisi hizo ni wazoefu katika shughuli za ukusanyaji wa mapato na madeni.

Anasema anaomba watumiaji wa kazi za wasanii na wananchi kushirikiana katika kazi hii, kwakuwa anaamini kazi za sanaa ni kazi kama kazi zingine ambapo wasanii wanapaswa kulipwa kwa kile wanachokitolea jasho.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi