Tuesday, October 3, 2017

Ray anaamini Teknolojia ya 'App' bado kwa wasanii



BAADA ya tasnia ya filamu ya Bongo Movies kuyumba mwigizaji wa filamu nchini Vicenti Kigosi ‘Ray’ amesema bado hana imani na kuuza kazi yake katika mtandao ‘App’  kutokana na ubora.

Ray anasema tayari alishapitia ‘App’ mbalimbali za Tanzania, lakini akagundua unaweza kupakua katika simu yako lakini ikashindwa kuangalia video kwa utulivu sababu zinakwama sana.

Alisema teknolojia yetu bado haina uwezo wa kumfanya mtu akatizama vizuri filamu kwenye simu baada ya  kupakua ‘app’  kama ilivyokuwa kwenye Cd.

Wasanii ambao tayari wameshafungua ‘app’ zao na kuweka filamu zao huo ni Ahmed Salim ‘Gabo’ ambayo anamiliki ya Uhondo na Wema Sepetu ambayo hivi karibuni ameweka filamu ya Heaven Sent.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi