Shamsa Ford
aanatarajia kuingiza sokoni filamu mpya ya Sikujua akiwa na mwigizaji Salm Ahmed ‘Gabo’ huku
akishikiria kwamba sasa hivi hawauzi haki miliki.
Wawili hao waliweza kufanya vizuri katika filamu kali kama Bado Natafuta ambayo ilimtambulisha Gabo katika ulimwengo wa filamu hadi leo jina lake kuendelea kung'ang'ania juu.
Akizungumza filamu
hiyo Shamsa itakayoingia hivi karibuni
hatouza haki yake isipokuwa kuna mtindo mpya wa kugawana mapato na msambazaji
bila ya kununua haki.
Alisema kwa
sasa hataki kuweka wazi ni njia gani ambayo kampuni hiyo mpya ya Kibalazani
huitumia, lakini anaamini kwamba atapata manufaa na haki yake pia itabaki.
Anasema
anaamini awamu hii ya pili ya uingiaji sokoni wa filamu utaweza kuwanufaisha
wasanii.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi