Tuesday, September 26, 2017

MAKALA; Soba ipi Sahihi?



Na Mohamed Mussa
KUTOKANA na mfumo wa maisha ya sasa ulivyo kila mtu amekuwa akiangalia kile kinachotokeza mbele yake na kukiona kama fulsa ya kujipatia kipato.
Hali hiyo imelekea wahitaji huduma  kutojua hasa wapi sehemu husika ya kupata huduma ambayo wamekuwa wakiitaka kutokana na matatizo  yanayowaandama.
Lakini hali imezidi kuwa mbaya zaidi baada ya baadhi ya watu kuchukulia  ni fulsa hata vitu vya msingi ambavyo havikuhitaji mzaha na ndipo husababisha matatizo kuongezeka zaidi badala  ya kupungua.
Zamani nilikuwa tukijua matatizo kama ya watumiaji wa madawa ya kulevya, yanahitaji uangalifu wa hali ya juu sana sababu watu hao sio wanakuwa hatari tu kwa wale wanaoishi nao ila huwa hatari hata kwa wao wenyewe.

Wapo ambao walikuwa na malengo sahihi ya kutaka kuwasaidia kwa kufungua vituo stahiki kwaajili ya kutoa huduma maarufu kama Soba, lakini kwa sasa mambo yamebadilika.
Leo vituo vya Soba vimekuwa vingi na kufanya watu washindwe kujua hasa ni kipi kituo sahihi kwaajili ya kusaidia waathirika.
Matukio kama hayo yalishawakuta waanzilishi wa vituo vya watoto waishia katika mazingira magumu, baada ya watu kuanzisha vituo kila mahali na kupelekea watu kutokuwa na imani na vituo hivyo
Mwandishi wa makala hii, alimfuata mwazilishi wa soba ya Pili Missanah Foundation na mwenyekiti wa  chama cha wamiliki Soba Tanzania ‘ Voice of Soba’   Pili Missahn ambapo alifafanua zaidi jinsi wanavyoweza kukabiliana na matatizo hayo

wanawachukulia ni wezi,” alisema..




Anasema mara nyingi jamii imekuwa ikipamba  kuhakikisha Soba zinaondolewa katika maeno yao, ingawa waathirika wanakuwa hawana madhara kwakuwa hawatoki nje kwa takribani miezi tatu hadi sita.
Pili anasema wamekuwa wakisaidia  watu wengi sana kupitia soba, lakini wanakabiliwa na hali ngumu ikiwepo kulipa kodi ya nyumba kwakuwa hawawezi kuchukua nyumba lazima wakodi nyumba nzima.
Anasema hata hivyo wamekuwa wakipata huduma mbalimbali kutoka Serikali na kwenye mashirikika makubwa, hivyo mtu anapopata tatizo  huwa wanajiongeza zaidi kwaajili ya matibabu.
Pili Missanah histori yake ya kuanzisha vituo hivyo ilianza mkoani Mwanza ambapo alizaliwa akiwa na kabira la  Msukuma, ambapo alimaliza  elimu yake ya sekondari Mwanza secondary mwaka  2003.
Baada ya hapo akajiunga na vituo vya kulelea watoto waishio katika mazingira magumu,  huku akiendelea na masomo yake ya IT.
Mwaka 2006 akajitolea kupita mtaani kwaajili ya kuongea na waathirika wa madawa ya kulevya na kuwapa ushauri, ingawa hakuwa na uwezo wa kusaidia chochote.
Mwandishi wa makala hii Mohamed Mussa Gomesa, akiwa na mwanamuziki Hawa maarufu kama Hawa Nitarejea au Hawa wa Diamond

Ndipo alipokuja Dar es salaam ambapo mwaka 2012 alipoamua kufungua kituo Kigamboni, kwaajili ya kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya.
Baada ya kufungua kituo cha kwanza Kigamboni aliseza kupata msaada kutoka kwa  Zacheria Hans Pope,  ambapo tayari alikuwa na vijana zaidi ya 700 waliweza kujitokeza kupata huduma hizo.
Watu kutoka makanisani na misikiti pia walianza kujitolea, hadi pale Hans Pope alipoamua kuachana na kituo hicho kutokana na hali yake ya kimaisha.
Anasema hata hivyo kituo kiliendelea kukua ba  kuzaa vituo vingine  vinne wakati huo vituo vitatu vikiwa Dar es Salaam pekee na kituo kimoja kikiwa Mwanza kipo kimoja.
Anasema Soba za Dar es Salaam hadi sasa ina  jumla ya waathirika  tofauti tofauti 93 wakati kituo cha Mwanza kina waathirika tofauti tofauti  29.
Alisema kituo hicho kina wafanyakazi wanaosimamia kituo wa kudumu ni  watatu wengine 18 wanakuja na kuondoka kwaajili ya kusaidia shughuli za kituoni.
“Kuna kipindi tunahitaji baadhi ya watu kutusaidia, sababu hali inakuwa tofauti,” alisema.

Anasema hadi sasa kituo kimesaidia watu 1977 lakini watu zaidi ya 200 wamerudia tena katika utumiaji, lakini wapo ambao wamearudia katika utumiaji wa madawa ya kulevya na baadaye wakaona ni bora kurudi tena kituoni kwaajili ya kumalizia dawa.
“Wengine wanakuwa wanaletwa na familia zao, hivyo wanaleta tabu na kusema kwamba akitoka hapa anaenda kutumia tena,”alisema.
Anasema kituo pia kimekuwa kikipokea watu wenye majina, wafanya kazi, watu maarufu na wasanii ambao hawataki kutajwa majina yao wanakuja  kituoni kwaajili ya kupata ushauri na elimu juu ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya ikiwemo pombe kali.
Pili anasema kituoni hapo miongoni mwa huduma wanayoitoa ni  elimu ya mtu kujitambua na ni jinsi gani unaweza kuishi bila ya kutumia kilevi chochote.
Anasema sio ngumu kwa muathirika kuamua kuchana na madawa ya kulevya kama akiamua yeye mwenyewe, kwakuwa atapata maumivu  kwa muda wa siku tatu baada ya hapo anakuwa sawa.

Anasema  hawatumii dawa kwaajili ya kuwaachananisha na madawa ya kulevya, isipokuwa  wanawapa elimu, ushauri na kuwafungia ndani ili wasiweze kutumia madawa hayo jambo ambalo wanafanikiwa kuwasaidia pia.
Kuwaachisha utumiaji wa madawa kunaendana na mpango maalumu wa unaojulikana kama ROSC , yaani uachaji wa kutumia madawa ya kulevya bila ya kutumia dawa.
“Huo mpango unasaidia sana watu kuwafanya wajitambue, kwakuwa tunaenda kwa vipindi na huwa hawatoki nje,” alisema.
 Anasema kwa sasa wamekuwa wakipata msaada kutoka Serikalini,  kwenye mamlaka ya kupambana na madawa ya kulevya na mashirikika mengine likiwemo shirika la umoja wa mataifa.
Lakini wanahitaji huduma zaidi kutokana na matatizo ambazo yanawakuta wakati mgonjwa anapozindiwa.
Mwisho by Mohamed Mussa Gomesa  (Habari Leo)

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi