Tuesday, September 26, 2017

MAKALA NDOA; Sababu wanaume kuishiwa nguvu za kiume



Kupungukiwa kwa nguvu za kiume sio suala la siri tena kwa vijana wa kisasa wa Tanzania, ila limeshakuwa tatizo kubwa kiasi cha kuligusa hasa Bunge letu kwa kulijadili suala hili japo kidogo, lakini wengi hawana elimu kwanini wamekuwa wakipoteza nguvu zao.

Kushindwa kwa uume kusimama pia hutambulika kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenza wake. Pamoja na ukweli kuwa mara zote Mwanaume lazima atafika kileleni, hali huweza kuwa tofauti kwa upande wa pili kwani mwanamke anahitaji mwanaume akawie zaidi ili na yeye (mwanamke) aweze kutosheka.

Mkeo hupendelea ukawie na ikiwezekana ukawie zaidi. Kama utakuwa unawahi kumaliza, basi mkeo anakuwa hapati raha kamili.
Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wanakabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni au kupungukiwa kwa nguvu za kiume. Hata hivyo kutambuwa tu kwamba wanaume wengine pia wana tatizo kama lako siyo sababu ya wewe kukaa tu bila kutafuta suluhisho la tatizo lako.
Habari njema ni kuwa zipo njia zinazoweza kuleta matokeo mazuri na hatimaye kulimaliza tatizo hili bila madhara mabaya hapo baadaye.
Wakati mwingine uume kushindwa kusimama inaweza kuwa si tatizo, lakiini jambo hilo linapojitokeza kila mara na kwa kipindi kirefu inaweza kuleta msongo wa mawazo kwa mume na hata kwa mke. Sababu nyingine amabzo zinaweza kupelekea uume usisimame vizuri ni pamoja na matatizo ya mhemko kama;
  1. Wasiwasi
  2. Hasira
  3. Msongo wa mawazo (Stress)
  4. Huzuni
  5. Hofu na mashaka
  6. Kukosa hamu ya tendo la ndoa n.k
Ili uume usimame vizuri ni lazima:
  • Mfumo wako wa neva uwe  na afya nzuri inayopelekea mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.
  • Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa
  • Misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa
  • Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.
Uume kshindwa kusimama vizuri kunaweza kusababishwa pia kama kipengele kimojawapo hapo juu hakifanyi kazi vizuri. Mambo mengine yanayopelekea kupunguwa kwa nguvu za kiume, uume kushindwa kusimama vizuri na kuwahi kufika kileleni ni:
  1. Uzee
  2. Kisukari
  3. Kujichua/Punyeto
  4. Uzinzi
  5. Kukosa Elimu ya vyakula
  6. Kutokujishughulisha na mazoezi
  7. Shinikizo la juu la damu
  8. Ugonjwa wa moyo
  9. Uvutaji sigara/tumbaku
  10. Utumiaji uliozidi wa kafeina. Na kama hujuwi kafeina ni kitu gani, bonyeza => hapa.
  11. Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
  12. Madawa ya kulevya
  13. Kupungua kwa homoni ya testerone
  14. Athari kutoka kwa baadhi ya dawa
  15. Pombe

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi