Wednesday, September 27, 2017

Nafasi ya Batwoman inamnukia Priyanka Chopra



NYOTA ya mwigizaji  wa Hollywood na Bollywood Priyanka Chopra inazidi kung’aa baada ya mashabiki zake kumtaja zaidi kwamba anapendeza zaidi kucheza katika filamu ya Batwoman and Spider – Woman ya nchini Marekani.

Chopra ambaye anafanya vizuri zaidi katika filamu za Marekani, mashabiki wameendelea kumpendekeza acheze kama Selina Kyela maarufu kama Catwoman katika mfulurizo wa Gotham City Sirens.
Hata hivyo taarifa zaidi juu ya mwigizaji huyo kama kukubaliwa kuchukua nafasi hiyo bado haijajulikana.

Mwigizaji huyo kwa sasa yupo na shirika la Umoja wa Mataifa akitembelea nchi mbalimbali, kwaajili ya kuwatembelea watu wenye matatizo wakiwemo watoto waathirika wa vita vya  Syria.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi