Monday, September 25, 2017

Mvua zamtia hofu Amitabh Bachchan



Huenda ikawa ni hofu kutokana na mvua na ngurumo zinazoikabiri  katika jiji la Mumbai, mwigizaji mkongwe wa filamu Bollywood, Amitabh Bachchan ‘Big B au T 2552’ amesema chanzo cha mvua hizo sababu mungu amekasirika.

Bachchan ambaye anaushawishi mkubwa katika nchi ya India, aliandika kupitia akaunti yake ya Twitter akiwataadharisha watu kutotoka nje kutokana na mvua hiyo kuto nyamaza kunyesha.
Ameendelea kusisitiza kwamba ngurumo za radi na miale mikali ya radi, ni salama zaidi kwa mtu kubaki ndani kuliko kudharau jambo hilo.
Alitoa onyo pia kwa Serikali yake kwamba  hakuna mtu ambaye anaweza kupambana na majanga asili kama Kimbunga Kizito, hata zile nchi ambazo zinanguvu zaidi Duniani.

Mvua hizo zilipelekea baadhi ya shule na vyuo kufungwa kwa muda, huku baadhi ya maeneo yakikubwa na mafuriko katika mji huo

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi