Monday, September 25, 2017

Bongo Movies hawajitambui



Mwigizaji  wa filamu na mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema ingawa amekaa kimya kwenye tasnia ya filamu lakini anajipanga kurudi upya na kazi nzuri kwakuwa Bongo Movies kaona hawajitambui.

Shilole  ambaye anaamini kwamba wasanii kuwa na kampeni nyingi ni sawa na kutojitambua, sababu hawajui wanataka nini.

Shilole ambaye anafanya vizuri na wimbo wake Kigoli,  anamikakati ya kuwekeza fedha nyingi kwenye mradi wake wa filamu kwakuwa hataki kurudia makosa yale yale wanayofanya waigizaji wa filamu.

Aamewataka waigizaji wenzake kutorudia stori, maeneo na kila kitu katika filamu zao ndio maana soko la filamu za nje likachukua nafasi kwakuwa soko la ndani kama lilibaki wazi.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi