Wauigizaji nguli wa filamu Bollywood nchini India Mithun Chakraborty na Shilpa Shetty wanatarajia kukutana katika
msimu wa pili wa kipindi maalum cha luninga cha Super Dancer 2 .
Shilpa
ambaye mara kwa mara amekuwa akiongoza kipindi hicho akisaidiana na majaji
wawili Anurag Basu na Geeta Kapur katika
msimu wa awamu ya kwanza.
Lakini
Chakraborty yeye alikuwa katika kipindi cha The Drama Company ambavyo vyote vinarushwa
katika Channel moja ya Luninga ya nchi hiyo.
Mithun ameendelea kutajwa na kuitwa katika vipindi vingi vya kucheza dansi,
kutokana na umahiri wake na kuwa miongoni mwa wachezaji bora.
Hivyo katika
msimu wa pili wa kipindi cha Super Dancer kitaongozwa na majaji wanne, akiwemo Shipa Shetty,
Chakraborty, Kapur na Basu .



No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi