Tuesday, September 26, 2017

Baada ya Diamond sasa Hamisa Petitman

Wakati vugu vugu la mwanamuziki Diamond Platnumza baba wa watoto wa tatu na Hamisa Mobetto likifika ukingoni tayari mavitu mapya yameendelea kumuibukia Hamisa Mobetto baada ya kusambaa picha yake akiwa na shemeji wa Diamond Platnumz mume halali wa Esma Platnumz wakumwitaga Petitman Wakuache wakiwa katika Malove.

Hata hivyo ili kuokoa ndoa yake, Petitiman amekanusha picha hiyo na kusema ni zamani.

officialpetitman_wakuachetzPicha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni za zamani sana. Hazina uhusiano wowote na maisha yangu ya sasa au na yale yanayoendelea kuhusu Hamisa ambaye anaonekana pia katika picha hizo kwa sasa.
Yeyote ambaye ameamua kuzisambaza ana nia moja tu. Kuniunganisha katika suala ambalo sihusiki na kunichafua. Mimi kwa muda mrefu niko na mke wangu mpendwa ambaye kila mtu anamjua na tuko busy kujenga familia yetu. Inawezekana jambo hili haliwafurahishi baadhi ya watu hivyo kuamua kusambaza picha za zamani kwa nia zao ovu.
Niseme tu kwa kifupi hizo picha sio za kutilia maanani. Ni picha za zamani sana. Kwa sasa sio muda wa kuchafuana. Huu ni muda wa kila mmoja wetu kupambana kujijenga na kulea familia yake. Mimi kama baba wa familia jukumu langu ndio hilo.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi