Na Mohamed
Mussa
TANGU siku
ya kwanza ilipotangazwa kuvunjika kwa bendi ya Yamoto, mwanamuziki kiongozi wa
bendi hiyo Aslay Isihaka amekuwa akiachia nyimbo na video mpya kila kukicha na kuzua
maswali mengi.
Mashabiki wa
bendi hiyo na mwanamuziki Aslay wengi wamekuwa wakijiuliza na kufikiria kwamba
mwanamuziki huyo huenda alijiandaa kuachana na bendi hiyo ndio maana aliamua
kuandaa nyimbo nyingi ambazo zinaingia sokoni sasa.
Aslay
anasema hadi sasa tangu walipoachana na bendi hiyo Machi 2017, walipotembelea
nchi saba za Ulaya tayari ameshatoa nyimbo 12 na bado anatamani kutoa nyingi
zaidi.
Kwa sasa
Aslay anafanya kazi na meneja Yusufu
Chambuzo ambaye ni mwaasisi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe pia ni mwalimu na mwazilishi
wa Yamoto Band.
Akizungumza
na mwandishi wa makala hii, Chambuso
alianza kufafanua kwa kusema yeye, Amani
Temba na Saidi Fella ndio walioanzisha kituo cha Mkubwa na Wanawe mwaka 2012 .
Kwa mara ya
kwanza kituo hicho anasema kiliundwa na watu wanne akiwemo na Suresh maarufu
kama Mr India anayemiliki studio ya Eyooo ambaye alitengeneza kazi za Bibi
Cheka na Dogo Aslay nanda kusema kwa
mama.
Anasema
kutokana na kukosa maelewano na Suresh alijitoa na kituo hicho kuendelea na
kazi zake mpaka ilipokuja kuibuka makundi mengi ikiwemo Yamoto.
Anasema
kufikia machi 2017 baada ya kurudi
kutoka kufanya matamasha katika nchi saaba za Ulaya, wasanii walianza
kulalamika kwamba wanahitaji kufanya kazi kujipima uwezo wao.
Anasema
kikubwa kwamba kila msanii alihisi kipato alichokuwa akikipata kilikuwa hakimtoshi,
hivyo alihitaji nafasi ya kufanya kazi zaidi.
“Ilinichanganya
sana kwakuwa mimi nilitumia muda mwingi wa maisha yangu katika kuandaa wasanii
kama Yamoto, lakini leo wanataka kugawanyika huku nikiwa sijapata chochote,”
alisema.
Chambuso
anasema yeye ndio mtu ambaye alikuwa akiwafundisha wanamuziki wa Yamoto,
kwakuwa alikuwa na ujuzi na alishapitia
bendi mbalimbali za muziki hadi
bendi za muziki wa asili.
“Mimi
nimeimba sana katika bendi, hivyo ninaweza kupiga ngoma, gitaa, kinanda tumba
na vifaa vingine huku nikiwa na uelewa mkubwa wa muziki,” alisema.
Anasema
ujuzi huo aliamua kuutumia kwaajili ya kuwafundisha Yamoto, kwakuwa aliamini mafanikio ya bendi hiyo kungeweza kumletea manufaa katika
maisha yake badala yake ikawa tofauti.
“Kwakuwa
wasanii walitaka kutengana kila mtu kufanya kazi yake uongozi tulikaa chini, tukapitisha wacha wafanye ili
wawe huru,” anasema.
Anasema
baada ya Yamoto kutawanyika kwaajili ya kutafuta maslahi nje ya kundi, aliamua
kuachana na muziki na kuamua kufanya kazi zingine.
Anasema kwa
muda wa miaka yote hiyo hakuna ambacho anakimiliki, kutokana na muziki ingawa
alikuwa kiongozi wa juu mwanzilishi na na mwalimu.
Anasema yote
hayo yalitokana na uongozi mbaya waliokuwa nao ingawa muziki ulikuwa ukiingiza
fedha nyingi.
Chambuso
anasema hataki kusema kwamba anamlaumu Saidi Fella, kwakuwa ndio mtu
aliyemfundisha njia za uongozi ingawa anatamani kuja kuwa kiongozi mzuri.
Anasema ingawa
bendi hiyo ilikuwa ikifanya vizuri
wanamuziki hawakuwa na chochote
cha kujivunia, ndio maana wakatamani kufanya maisha ya kujitegemea.
Baada ya
kutoa wimbo wa mwisho wa Basi, kila
mmoja alianza kuhangaika kivyake ili aweze kuongeza Kipato, ndipo Aslay
alipoachia nyimbo kama , Kidawa, Angemuona na Tete ambapo zilianza kufanya
vizuri.
“Baada ya kutoa
nyimbo hizo alinifuata na kuniambia kwamba ananihitaji kwaajili ya kufanya kazi
ya pamoja,” anasema.
Anasema
aliamua kuungana naye ambapo walifungua ofisi, lakini muda huo huo mtayarishaji
wa muziki wa Yamoto Shirko naye aliwafuata na kutaka wafanye kazi pamoja.
Wanamuziki
wengine akiwemo mwanamuziki wa Zanzibar Berry Black, Osama, Podo, Kingo Master
na K Young wote walikuwa Mkubwa na Wanawe waliahama kumfuata.
“Nilipoona
wanakuja wengi niliwasimamisha na kuwaambia hata hii ni sawa na Mkubwa na
wanawe kwakuwa uongozi ni ule ule ,” alisema.
Alisema muda
mchache wakafungua ofisi na kupata vifaa na tayari wakaanza kufanya kazi kwa
wingi.
Meneja
Chambuso amesema bado yupo katika kituo cha Mkubwa na Wanawe, kwakuwa haki zote
za umiliki bado zipo pia anatoa msaada wa ushauri kwa wasanii wa kituo hapo.
Lakini
mwisho pia alisema nyumba ambazo wanamuziki wa Yamoto walizopewa ni za kwao
kweli, isipokuwa kukamilisha kupewa nyumba hizo ndio bado hadi leo.
Pia
mwanamuziki Aslay Isihaka ambaye kwa sasa anajiita Dingi Mtoto, alifafanua
zaidi anasema aliamua kufanya kazi na meneja Chambuso kwakuwa ndio mtu
anayeujua mziki wake.
“Baada ya
kila mwanamuziki kutaka kufanya kazi kivyake niliona bora nifanye kazi na
Chambuso kama meneja wangu, sababu yeye ndiye aliyenipokea na kunifundisha
muziki,” alisema.
Anasema kwa
sasa hana ugonvi na mwanamuziki mwezake wa Yamoto kwakuwa hawakuachana kwa
ugonvi na kilichopelekea kutengana kwa muda ni kutokana na maslahi ya kazi zao.
Alisema hivi
sasa wanastudio na ofisi Mwembe Yanga Temeke, ambapo mara ya kwanza alitamani
kitu hicho kiwe Sinza lakini ilishindikana.
“Nilipata
nyumba Sinza wakanikubalia lakini nilipowaambia anataka kufungua studio ya
Muziki walikataa, ikabidi ofisi tuhamishie Temeke Mwembe Yanga,” alisema.
Alizitaja
nyimbo ambazo alizitoa baada ya kutoka Mkubwa na Wanawe kuwa ni Kidawa, Tete,
Rudi, Mario, Angekuona, Autegeki, Ndoa, Likizo, Baby, Danga, Pusha na Mhudumu.
Alisema hadi
sasa ananyimbo zaidi ya 32, ambazo bado hajazitoa na yupo katika mikakati ya
kuzitoa.
“Malengo yangu
nikuufikisha muziki wangu mbali zaidi, najiona nimekuwa mpya kwakuwa najiamini
kwa sasa,” alisema.
Anasema
tayari ameshaanza kutambulika zaidi kwa kazi zake na tayari amekuwa akipata
matamasha mengi mkoani na Dar es Salaam.
Alisema kwa
sasa amekuwa na mendeleo kidogo kwakuwa aliondoka kwaajili ya kutafuta
maendeleo, ambayo kwa sasa anayaona japo kidogo.
Wakati huo
huo Meneja Chambuso amesema kwa sasa amefanikiwa kunua gari dogo kwa muda wote
wa maiasha yake ya kimuziki, jambo ambalo anahisi anaanza kupata nafuu kwa kile
ambacho alikuwa akikifanya kwa miaka yote.
Mwisho
By Mohamed M Gomesa (Habari Leo) 0714956288


No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi