Wednesday, September 27, 2017

Diamond afuta neno Kichwa cha Mwendawazimu

Wakati zamani tulikuwa tukiona kama ni kitu ambacho hakiwezekani wanamuziki wa nje kuomba urafiki au kutafuta chochote kwa wanamuziki wa ndani, kichwa hicho cha Mwendawazimu katika muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz amekivunja na sasa tunaona mabadiliko makubwa kwa muziki wetu chini ya kaptain wa jahazi la WCB.

 Baada ya Dj Khaled kumfollow na rapper Rick Ross kumpost hitmaker huyo wa Eneka kwenye mtandao wa Instagram, mume wa mwanamuziki wa Marekani mpiga kinanda mzuri Alicea Keys, Swizz Beatz na yeye ameamua kufuata nyayo kama hizo,
Huenda hii inaweza kuwa sababu ya milango kufunguka, kwa wanamuziki wa ndani.
Swizz alionekana akiwa pembeni ya mrembo wa dunia Flevian Matata wakifurahi, na kupost kipande cha video akilitaja jina la Diamond Platnumz.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi