Wednesday, September 27, 2017

Brad Pitt alipoungana na Shah Rukh Khan



MKALI wa Bollywood na Brad Pitt ameamua kushirikiana na mkali wa Bollywood Shar Rukh Khan kwaajili ya kuitangaza filamu mpya ya War Machine katika jiji la Mumbai.

Pitt ‘53’ alikutana na SRK kwaajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali yakiwemo ya filamu, pamoja na kufanya shughuli mbalimbaali zinazohusiana na filamu na kutengeneza ukaribu wa kazi.
Katika filamu hiyo ambayo inazungumzia tukio la kweli ambalo liliwahi kutokea, imechezwa pia na waigizaji Ben Kingsley, Tilda Swinton, Anthony Michael Hall na Topher Grace na kuongozwa na David Michod.
Alisema filamu hiyo ambayo imechezwa katika nchi ya Afghanistan imetoka katika kitabu cha  The Operators: The Wild & Terrifying kilichoandikwa na Michael Hastings.

Alisema yeye aliigiza kama Kamanda wa jeshi la Marekani mwenye nyota nne akitumia jina la  general Glenn McMahon, aliyepambana vita kati ya Marekani na Afghanistan.
Mvua hizo zilipelekea baadhi ya shule na vyuo kufungwa kwa muda, huku baadhi ya maeneo yakikubwa na mafuriko katika mji huo.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi