MAMLAKA ya chakula
na dawa –TFDA, kanda ya kati imeteketeza zaidi ya tani tatu za shehena ya
vyakula, vipodozi vifaa tiba na dawa zenye thamani ya shilingi milioni 38. 8
kufuatia msako mkali
uliofanywa katika maduka yaliyoko Manispaa ya Dodoma na
kubaini bidhaa hizo hazifai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kumalizika
muda wa matumizi pamoja na kuwa na kemikali zenye viambata vya sumu.
Meneja wa TFDA Kanda ya Kati, Florent Kayombo amesema bidhaa
hizo zimekamatwa kufuatia msako uliofanyika mwezi Jully na August ambapo pia
jumla ya maduka tisa ya vipodozi yalifungiwa na kutozwa faini.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi