Sir Elton John amesema angependa sana kukutana na Vladimir
Putin wajadiliane kuhusu alichosema ni mtazamo wa kushangaza wa kiongozi huyo
wa Urusi kuhusu haki za mashoga.
Ripoti
ya shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch mwaka uliopita
iliishutumu Urusi kwa kushindwa kuzuia mashambulio dhidi ya watu wa makundi
yanayobaguliwa na kutochukulia hatua wanaotekeleza mashambulio hao.
Akiongea
na BBC, Sir Elton amesema angefurahia sana kukutana na Putin ingawa anajua
kwamba baadaye huenda kiongozi huyo akamcheka na hata kumuita mpumbavu.
Mwanamuziki
huyo kwa sasa yuko Ukraine ambako alihimiza kuwepo kwa haki zaidi kwa mabasha
na wasagaji.
Urusi,
ambayo ni jirani wa Ukraine, Juni 2013 ilipitisha sheria iliyolenga kuadhibu
watu binafsi wanaoendeleza “tabia za ushoga miongoni mwa watoto”.
Sir
Elton alishutumu hatua hiyo, pamoja na matamshi ya Bw Putin aliyoyatoa mwaka
jana, akiashiria kuwa mashoga waliwaandama watoto.
“Wewe
ni Rais wa Urusi, na unasema jambo la kipuzi kama hilo?”
Alisema
mtazamo wa Putin kuhusu mashoga ni wa “kuwatenga na kuwabagua” na wa
“kushangaza”.
"Ningependa
kukutana na [Bw Putin]," Sir Elton aliambia mwandishi wa habari wa masuala
ya kidiplomasia wa BBC Bridget Kendall.
"Huenda
akanicheka baadaye, na kuniita mpumbavu, lakini angalau nitakuwa nikijua kwenye
dhamiri yangu kwamba nilijaribu.”

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi