HUENDA ikawa hii ni nafasi nyingine kwa
wapenzi, waandaji na watizamaji wa filamu nchini kwenda kuhudhulia Tamasha la
Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) ambalo linafanyika kila mwaka katika kisiwa
cha Zanzibar na kutambulika zaidi kwa jina la tamasha la Majahazi .
ZIFF ni
miongoni mwa matamasha makubwa nchini
huenda likawa kubwa zaidi kwakuwa linakutanisha wadau wa tasnia kutoka Afrika
na Dunia kwa ujumla, huku likionesha filamu tofauti .
Lakini
kikubwa lazima ifike tujiulize maswali baada ya mwaka huu kuwa ni msimu wa 17, tangu ilipoanzishwa kwake je! inasaidia kukuza tasnia ya filamu Tanzania na
kitu gani zaidi wasanii huwa wanakipata kutoka ZIFF.
Akizungumza
na mwandishi wa safu hii hapa Bongo Unit, Meneja wa Tamasha la ZIFF, Danniel Nyalusi , amesema
mwaka huu kidogo tasnia ya filamu za hapa Tanzania imejitahaidi kwa kiasi
kikubwa ingawa si sana kuingingiza filamu zao katika tamasha hilo.
Alisema
filamu ambazo zimewafikia kutoka Tanzania ni filamu 30, ambapo zimekaguliwa na
kupatikana filamu 16 ambazo ndizo
zilizofanikiwa kuingia kuwania nafasi mbalimbali katika kipengele cha
tuzo za Zuku Bongo Movie .
Alizitaja
miongoni mwa filamu ambazo zimeingia katika kipengele hicho ndani ya mabano ni
mwongozaji wa filamu hiyo.
Filamu ya
Mapenzi ya Mungu (Alex Sponga), Mr Kadabanja (Adam Kuambina), Fundi Selemala
(Issa Mussa ‘Cloud 112’), Mbwa Mwitu
(Leah Mwandemseke), Dady’s Wedding
(Honeymoon Algebri), V.I.P (Vicent Kigosi), Single Ziro (Timoth Conrad),
Pishu (Leah Mwendemseke), Samaki Mchangani (Amil Shivji), Kutakapokucha (Simon
Mwakifamba), Msago (Haji Usi), Mikono Salama (Jacob Stephan), Nyange Kigoma
(Saidi Hemed Ally), Going Bongo, Kilimo 2 na Faraja.
Nyalusi
alisema pia zipo filamu tano, ambazo zimeingia kuwania nafasi za filamu za
Kimataifa ambapo zamani wasanii wa Tanzania walikuwa wakiogopa kabisa kuwania
nafasi hizo.
Filamu hizo
ni Single Ziro (Timoth Conrad), Pishu (Leah Mwandamseke),Kutakapokucha (Simon
Mwakifamba), Mr Kandabanja (Adam Kuambiana), Daddy’s Wedding (HoneyMoon Algebri).
Alisema filamu
16 kati ya 30 ndizo pekee zilizofanikiwa kuingia na filamu 14 zilishindwa
kuwania tuzo hizo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wa filamu kukosa ubora
na lingine filamu moja kuwa na sehemu mbili ‘part 1 na part 2’.
Alisema
kulingana na soko la filamu Tanzania,
Dar es salaam peke yake kunazalishwa filamu zaidi ya 30 kwa mwezi mmoja
tu, lakini filamu zilizoletwa katika
tuzo hizo ni 30 kwa mwaka mzima.
Anasema
sababu inayopelekea kutoletwa kwa filamu hizo katika tamasha hilo, ambapo zaidi
ya kuoneshwa au kutangazwa kwa filamu pia kunampelekea msanii kujulikana
kimataifa.
Nyalusi
anasema sababu kubwa kwamba wasanii wengi wamekuwa wameuza haki zao, hivyo
kuepeleka filamu katika tamasha hilo, au lingine lolote wanaona ni sawa na
kuitangaza kampuni ambayo tayari alishamalizana nayao katika malipo.
“Wasanii
wanaamini hilo ni jukumu la kampuni katika kupeleka popote filamu hizo kwakuwa
wao tayari walishalipwa na kuza haki zao,” alisema Nyalasu.
Anasema hata
hivyo msanii kuuza haki yako sio kwamba ndio umeuza na jina la utengenezaji ,
hivyo tuzo ya mtayarishaji bora bado inarudi kwa msanii au mwigizaji bora jambo
ambalo anawasihi wapeleke kazi hizo.
Alisema hata
hivyo zaidi ya kujulikana yeye na kazi yake, lakini pia wanapata fulsa ya
kukutana na waandaji na waigizaji wa Kimataifa ambao tayari dunia inawafahamu
kutokana na kazi zao.
Anasema kwa
mwaka huu atakuwepo mwigizaji mkongwe ambaye alivuma na filamu ya Sarafina ya
Afrika kusini, Leleti Khumaro filamu ambayo ilikuwa ikizungumzia ukadamizaji
juu ya Waafrika wa Afrika Kusini.
“Mwaka huu
tumemleta yeye kwakuwa tunataka kuitambulisha Afrika zaidi hasa Pan Africa,
ndio maana tukamchague yeye,” alisema.
Alisema hata
hivyo walishawahi kuja wakali wengine ambao mchango wao katika soko la filamu
la dunia ni mkubwa kama Danny Glover (2009) ambaye alifanya vizuri katika
mfululizo wa filamu ya Leather Weapon akiwa na Mel Gibson na Jet Lee.
Wakawaleta
tena Mario Van Peebles (2012) ambaye anatambulika zaidi katika filamu ya Solo,
Danny Sheffer (2013 na 2014) anayeigiza
kama Mandela, na mwingine aliyefanya vizuri katika filamu iliyoitambulisha
Brazir katika soko la dunia Leonald Lun- Kang kupitia filamu ya City of God.
Wasanii hao
na waongozaji wa filamu sio kwamba wanakuja na kuondoka ila huwa wanatoa elimu
katika madarasa ambayo huandaliwa kwaajili ya masomo kuhusiana na filamu.
“Wasanii
wanapata mwaliko maalum kuhusiana na madarasa hayo, na wanapata elimu na hata
kuwasiliana na wasanii hao kuhusu ni jinsi gani ya kufanya kazi,” alisema
Danny.
Lakini Danny
alisema nafasi hiyo imeendelea kuwepo kila kukicha na kuwavuta wasanii na
waongozaji wakubwa, lakini kinachofanya tasnia ya filamu isifaidike ni kutokana
na wasanii wake kuwa waoga wa kuongea ingawa lugha wamekuwa wakiijua.
Lakini
mwisho kama mwandishi nilimaliza kwa kuongea na mwigizaji Vicenti Kigosi ‘Ray’,
ambaye ni miongoni mwa wasanii zaidi kwamba alikuwa akiudhulia tamasha hilo pia
ni mhudhuliaji nzuri wa madarasa ya elimu.
Akizungumza
na mwandishi Ray alisema kweli wamekuwa wakipata fulsa kubwa ya kuwaona au
kuwasiliana na waandaji wakubwa wa filamu duniani, lakini kitu ambacho
kinashindwa kufanya nao kazi kunatokana na bajeti ya filamu za Tanzania.
Anasema
wasanii wa kimataifa wanaamini bajeti ndogo ni shilingi milioni mia tano,
lakini wao filamu wanauza kwa milioni 50 jambo ambalo linawafanya wawaogope
waongozaji na wasanii wanaokuja katika matamasha hayo.
“Tunaishia
kupata elimu katika madarasa ambayo wanatoa elimu, na tunashukuru mungu
inatusaidia lakini lakini bajeti yetu hairuhusu sisi kufanya kazi nao,” alisema.
Alisema pia
anakubaliana na kwamba filamu nyingi huingia sokoni kila siku kiasi cha kufikia
30 kwa mwezi, lakini anasema filamu nyingi zinazoingia zinatokana na kila mtu
kutaka kuwa mtayarishaji na sio mwingizaji.
Anasema hali
hiyo inapelekea kila mtu kuzalisha filamu yake baada ya kuwa mwigizaji, hii
inatokana na makampuni kulipa kiasi kidogo ndio maana mtu anaona ni bora
kuzalisha filamu yake.
“Ndio maana
filamu zinaingia sokoni zaidi ya 3o, lakini hakuna hata moja yenye ubora hali
inayopelekea soko la filamu kuyumba kwa maana watu wanasema zote ni mbovu
kutokana na chache walizoziona,” alisema.
Mwisho
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi