Huenda ukawa hujui lakini nguli wa filamu nchini, Wiliam Mtitu alikuwa akimtegemea sana mwigizaji Adam kuambiana katika kazi zake za sanaa,
na kabla ya kifo chake alimwacha wakati ameikamilisha filamu , ambayo kwa Mtitu anahisi kama ni zawadi ya mwisho.
Aliiambia
Bongo Unit kwamba Stupid Father iliongozwa na kuchezwa na Kuambiana, ikafanya vizuri sokoni lakini kabla ya
kufariki alishakamilisha filamu nyingine ya Who is My Child.
Alisema filamu
hiyo ameamua kuingiza sokoni muda huu kama kumuenzi, rafiki yake huyo na mfanyakazi
mwenzake.
“Hakuna kama
Kuambiana katika kampuni yangu, bado pengo lake litakuwa kubwa sana” alisema.
Mtitu
alisema tangu alipoondoka Kuambiana hadi leo amekuwa akiangaika kumpata
Mwongozaji mzuri atakayeweza kuongoza filamu zake kama ilivyokuwa kwa msanii
huyo.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi