KIONGOZI wa
bendi ya Msondo Ngoma, Saidi Kibiriti
amesema bendi yake kwa sasa imetambulisha nyimbo mpya ikiwemo Nadhiri iliyotungwa na
Juma Katundu. Kibiriti
alisema muziki wa dansi hasa ule wa zamani umeendelea kupewa kisogo wa
waandishi watangazaji wa redio na luninga na kusababisha kudumaa.
Alisema sasa
hivi muziki uliopewa kipaumbele ni wa kizazi kipya, ambao umekuwa ukiingizwa
sauti na wanamuziki huku wakitohoa nyimbo za watu na kuzifanya za kwao.
“Wanahariri
kila kitu cha nje na kuziita nyimbo zao, kwanini wasishike vifaa wakapiga ili
tupate nyimbo zetu,” alisema Kibiriti.
Alivitaka
vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuweza kuunga mkono mziki huuo ili
kusogea mbele.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi