MSANII wa
muziki wa kizazi kipya, Elias Baranaba ‘Barnaba Boy’ amesema hatoruhusu mkewe
kuwa mwigizaji wa kuonekana katika video ya mtu
mwingine ingawa yeye mwenyewe
alimtumia katika video yake Wahalade.
Akizungumza
na mwandishi wa Bongo Unit, alisema alimtumia mkewe akiwa kama mshiriki wa video ‘model’ katika wimbo huo,
ili kuonesha ni jinsi gani anavyomsamini.
Lakini
amesema hatokubali mtu mwingine
kumchukua hata kama atamlipa ilikuonekana katika video yake, kwakuwa hataki mkewe
hajihusishe na sanaa yoyote zaidi ya biashara.
“Mke wangu
ni mfanya biashara na anabiashara zake, mimi nilifanya vile kama mwenyewe
lakini sitopenda afanye kwa mwingine,’ alisema.
Barnaba
alisema ingawa alikuwa ni mkewe pia yeye
ndiye aliyependekeza aonekanae kwenye video hiyo, lakini alimpia ingawa ilikuwa
ngumu kupokea hizo fedha.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi