MWIGIZAJI wa
filamu nchini Flora Mvungi, amesema amejiingiza rasmi katika tasnia ya muziki
wa kizazi kipya baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu
Alisema
kabla ya kuamua kujiingiza kwenye tasnia ya uigizaji, alishawahi kuwa mwimbaji
kipindi hicho akiimba pamoja na Kala Jeremiah kabla ya Bongo Star Search,
lakini hakuweza kumudu kwa muda mrefu sana kwenye tasnia hiyo, kiasi cha sasa kuamua kurudi tena.
Mvungi
alisema mwaka 2011 aliachia wimbo Sinaga, ambao ulikuwa kama wa mwisho kabla ya
kuamua kurudi tena kwenye tasnia hiyo safari hii.
“Nimeamua kuingia
kwenye muziki rasmi, natarajia kuachia
kazi zangu nyingi” alisema.
Alisema
wimbo wake mpya alioutoa hivi karibuni unaitwa Kidogo, ambao amemshirikisha
mumew, Khamisi Ramadhani ‘H baba’.
Alisema
mshirikisha baada ya maoni ya watu kumshauri kufanya hivyo kutokana na wote
kuwa na kipaji cha uigizaji na Uimbaji.


No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi