KIONGOZI wa bendi ya Coast Modern taarab, Omari Tego
amesema wanatarajia kufanya tamasha kubwa mkoani Tabora na mwanamuziki mwenzake
Hadija Kopa.
Tego alisema
tamasha hilo wanatarajia kufanya kipindi hiki cha sikukuu katika wilaya ya Urambo, baada ya hapo
wanatarajia kuzunguka na wilaya nyingine.
Alisema
bendi yake mara nyingi imekuwa ikikubalika eneo hilo, jambo ambalo anaamini
watafanya vizuri kwakuwa na wapenzi wengi.
“Tunakubalika
na ndio maana tunaarikwa kufanya tamasha eneo hilo, hivyo tunaahidi kutoa
burudani ya nguvu,” alsema.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi