MWIGIZAJI wa
filamu nchini Single Mtambalike ‘Rich Richie’ amesema hawezi kutoa filamu kila
mwezi kuhofia ‘kukopi’ filamu za watu na kusababisha kushuka kwa hadhi yake.
Aliimbia Bongo Unit alisema unaweza kumpa mtu kazi ya kuandika stori ili utengeneze filamu lakini bila ya kujua kama ameiba stori au kuibadili stori ya filamu nyingine.
Alisema hiyo ndio sababu inayopelekea filamu nyingi za kitanzania kufanana, jambo ambalo haitaji litokee kwake.
“Filamu
yangu mpya itakuja kwa jina la Kalekwa, lakini bado kukamilika ndio nipo kwenye
mikakati ya kuandika stori,” alisema.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi