BENDI ya
Twanga Pepeta, inatarajia kufanya mambo mapya katika sikuu hii ya Idd kwa kuachia nyimbo zake mbili na kutambulisha wanenguaji
wapya katika sikukuu ya Idd Mosi katika ukumbi wa Mango Gadern.
Akizungumza
mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka, alisema nyimbo wanazotarajia kutambulisha
siku hiyo ni Mapenzi yanaua uliotungwa na Haji Ramadhani na Ganda la Mua
uliotungwa na Sarehe Kupaza.
Alisema pia
kutakuwa na wanenguaji wa kiume na wakike ambao ni wapya, ambao nao
watatambulishwa kwa wapenzi wa bendi hiyo katika msimu huo wa sikukuu.
Asha pia amesema atafanya matamasha mawili moja likiwa Dar es salaam na Bagamoyo kwaajili ya mashabiki wa bendi ya
Twanga.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi