BAADA ya
kuachia wimbo wake mpya unaitwa Upendo, mwanamuziki Ben Poul anasema wimbo huo
umekuwa ukikuwa umaarufu polepole sana tofauti na nyimbo nyingine jambo ambalo limekuwa likimpa hofu.
Ben Poul alisema wimbo wake huo hauna tofauti na wimbo Jikubali alioutoa zamani, kwajinsi unavyosua
sua kukua kwake.
Alisema wimbo
huo mwanzo ulivyotoka alijikuta akikata tamaa na kuamini hautafika popote,
lakini kadri siku zinavyokwenda ndivyo ulivyozidi kupanda juu na kuwa maarufu.
“Wimbo wangu
wa Jikubali ulinikatisha tamaa, lakini sasa ndo naweza kusema wimbo uliokuwa na
mafanikio mkubwa kuliko zote,” alisema.
Alisema hii
inatokana na nyimbo zake, ni lazima mtu atulie na azisikilize kwa umakini.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi