Mwenyekiti
wa Bongo Movie Unit, Steve Mangele ‘Steve Nyerere’ amewataka wasanii wa filamu
na muziki kujiunga na mfuko kuweka kwa hiyari wa PSPF ili kuepuka kuomba
misaada wanapopata matatizo.
Akizungumza jana
katika semina iliyoandaliwa na mfuko huo wa kijamii, alisema wasanii wengi
wamekuwa wakifanyakazi bila ya kuwa na chochote ambacho kitawasaidia pindi
wanapata matatizo ikiwemo maradhi au
hajari.
Alisema wanakuwa
katika wakati mgumu wakati wa kuchangishana, jambo ambalo si zuri kutokana
na hali kuwa ngumu kwa sasa.
| (Mwigizaji Simon Mwapangate 'Rado' akiwa na Zuberi Mohamed 'Rado') |
Aliwataka kujiunga katika mfuko huo, ambao utasaidia
kutatua matatizo yanayowakabiri pindi yanapotokea na kupunguza tatizo la kuchangishana mara kwa
mara.
“Sisi
wenyewe mashahidi wenzetu wameugua na wengine kupata matatizo makubwa hadi
kupelekea kifo, tumekuwa tukijikamua kwa kiasi kikubwa ili kusaidia. Ni bora
tujiunge na mfuko huu ili tuweze kusaidiana pale tunapopaweza,” alisema Mangele.
Naye
mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Adam Mayinda alisema, mfuko huo zamani ulikuwa ukijishughulisha
na taasisi za Kiserikali na Waajiriwa wa makampuni makubwa.
Alisema
lakini sasa wameamua kutoa huduma hiyo kwa kila mtu, ili kuweza kunufaika
kipindi cha matatizo au pindi anapokwama au anapohitaji fedha zake kwaajili ya
jambo fulani.
| (Fatuma Makongoro 'Bi Mwenda) |
Alisema mtu
anaweza kujitoa katika mfuko huo,
kulipwa kiasi chake chote alichoweka bila ya kukatwa kiasi chochote.
“Sisi
hatufanyi biashara ila tunajaribu kuwasaidia watu kuweza kuhifadhi fedha zao,”
alisema Mayimba.
Alifafanua
zaidi kwa kusema mtu anaweza kujiunga kwa jia ya simu, pia akatuma fedha zake
popote kwa njia ya simu na hata kuangalia taarifa zake kupitia simu yake ya
mkononi.
Jenifer Kyaka 'Odama'
Vyonne Sherry 'Monalisa'
Mtunis
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi