
MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Emmanuel
Simwinga ‘Izzo B’ amesema ni kawaida yake kuachia wimbo mpya siku ya kuzaliwa
kwake Desemba 12, lakini mwaka huu hajajua atatoa kwa mtindo gani.
nyota huyo
ambaye kwa sasa anatamba na wimbo Love Me akiwa na Elias ‘Barnaba’ na Sarah
Kais Shaa, alisema kwamba ni kawaida kutoa wimbo kila inapofika tarehe hiyo,
isipokuwa uzinduzi wa wimbo ndio unatofautiana.
tayari ameshakamilisha nyimbo
nane, na kati ya hizo moja ndiyo inapaswa kutoka siku hiyo jambo ambalo
anaamini peke yake hawezi kuchagua bila ya wadau wake.
“Nina nyimbo nyingi nilizofanya ila nahitaji kukaa na watu wangu
ambao wananishauri na kujua ni wimbo gani niutangulishe kuutoa” alisema.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi