NAIBU waziri wa Kilimo Chakula na
Ushirika, Mheshimiwa Adam Kighoma
Malima, amewataka Watendaji na Viongozi wa Vyama vya ushiriki vya mkoa wa
pwani, kulipa 2 .5 bilioni kwa
kusababisha harasa na upotevu wa fedha za wakulima wa Korosho.
Akitoa tamko
hilo katika kijiji cha Kuruti, kata ya Chungubweni wilaya ya Mkuranga mkoa wa
Pwani, alisema katika msimu wa 2011 na 2012 wakulima wa Korosho mkoa wa pwani,
waliwasilisha madai ya kutolipwa fedha zitokanazo na biashara ya Korosho.
Alisema ndipo
wakamtuma Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika, aliendesha ukaguzi wa hesabu za vyama
vya Ushirika vya msingi (AMCOS)ambao ulithibitisha madai ya wakulima na kubaini
hasara na upotevu wa fedha hizo.
Aidha alithibitisha kwamba wahusika wakuu wa
upotevu wa fedha za wakulima ni Wajumbe wa Bodi na Watendeji wa Vyma husika vya
Ushirika.
Katika
ukaguzi huo kiasi cha sh.3,057,794,500, kilibainika kupotea kwenye vyama vya
Ushirika 97, na kiasi hicho kinahusisha deni la sh. 2,567,056300, la vyama 69
vya wilaya ya Mkuranga.
Mhe, Malima
alisema kwa mujibu wa kifungu cha 93 (2) cha sheria ya vyama vya ushirika ya
mwaka 2003, Mrajis wa Vyama Vya
Ushirika, aliandika Notisi za madai kwa kila Mjumbe wa Bodi na Mtendaji
aliyebainika kushiriki, katika hasara na upotevu.
Na kuwaamuru
kulipa fedha kulingana na hasara au upotevu uliojitokeza kwa kila AMCOS, ili
kulipa fidia au hasara walizosababisha.
Katika
notisi za Madai wahusika walielezwa haki ya kukata rufaa kwa Mhe. Waziri mwenye
dhamana ya Maendeleo ya Ushirika, ndani ya siku 30, kuanzia tarehe ya kupokea Notisi za Madai.
Alisema
baadhi ya wahusika waliamua kukata rufaa kwa Mhe. Waziri wa Kilimo Chakula na
Ushurika, wakidai kwamba wao hawakuhusika na hasara iliyotokana na uzembe na ubadhirifu uliokea,
hivyo kumuomba Mhe. Waziri wasilipe deni hilo.
Jumla ya
rufaa mia nne therasini nne(434)
ziliwasilishwa kwa Mhe. Waziri, ili kutendea haki kwa wahusika, uchunguzi wa
rufaa hizo ulifanyika kwa kuzingatia nyaraka zilizowasilishwa kwa Mhe. Waziri
wa Kilimo Chakula na Ushirika.
Hivyo
amekubaliana na maamuzi yaliyofanywa na Mrajis, Mhe. Waziri ameona kuwa hasara
hizo zimetokana na uzembe na ubadhirifu wa wajumbe wa Bodi na Watendeji kwa
kuidhinisha malipo yasiyo halali.
Hivyo Mhe.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, amezikataa rufaa zote na kuwaagiza, kila
Mjumbe wa Bodi na Mtendaji wa Chama cha Ushirika, kilichohusika kulipa deni kwa mujibu wa
Uchambuzi, uliofanywa na Mirajis ndani ya siku kumi na tano (15).
Kwa mujibu
wa sheria ya Vyma Vya Ushirika, ya Mwaka 2003, Mirajis atamchukulia mra moja
hatua za kisheria, za kumfikisha Mahakamani, hatua hizo za kisheria ni pamoja
na kumfungulia kesi ya jinai kwa kosa la ubadhirifu.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi