Miongoni mwa
filamu ambazo alifanya vizuri na kupata mashabiki wengi ni, Kivuli akiwa na
Wastara Juma, Waves of Sorrow ya Ray, Family War, I am Lost na nyinginezo.
Ndipo
mwandishi wa makala hii, alipoamua
kumtafuta ili kuweza kujua siri ya kuvuma kwake na mafanikio ya muda
mfupi, huku wengine wakimwona kama msanii mchanga.
Akizungumza
na mwandishi wa makala hii, anasema ni kweli katika tasnia ya uigizaji ni
mchanga, kwakuwa alianga kuigiza filamu yake ya kwanza mwaka2011 ambayo iliitwa
My Angel.
Anasema
katika filamu hiyo, alikuwa na Yusufu Mlela, na Hemed Seleman, na hapo ndipo
alipoamua kuanza kujikita zaidi katika tasnia hiyo.
“Mimi ni
mchanga katika tasnia, ingawa kabla ya hapo watu walikuwa wakinishauri niingie
kwenye tasnia hiyo nami nikawa nakataa” anaelezea.
Anasema
lakini katika tasnia ya filamu na muziki wa Bongo Fleva, yeye si mgeni sana
kwakuwa tayari alikuwa huko kwa muda mrefu sana.
Kipindi hicho
anasema alikuwa nyuma ya kamera, ambapo alikuwa akifanya kazi tofauti na ambayo
anafanya sasa baada ya kuja mbele ya kamera ambapo watu ndipo wanamuona.
Slim
anasema kwa mara ya kwanza baada ya
kumaliza mafunzo yake, akiwa Afrika Kusini katika shughuli zake za kikazi,
mwaka 2000 aliamua kusomea masomo ya muda mfupi kuhusiana na mambo ya
Video production.
“Nilikuwa
tayari nashulikia masuala ya production, hivyo nikaona ni bora nisomee ili
kuweza kuongeza ujuzi zaidi’ anasema.
Baada ya
kurudi nchini alipata kazi kwenye kampuni moja lakini hakukaa nayo sana na
baada ya hapo akaanza kufanya kazi kwenye kampuni mbalimbali za Production.
Kwa kipindi
hicho anasema alikuwa akijihusisha zaidi, na upigaji picha wa video, za
matangazo, muziki wa kizazi kipya na filamu kwa muda mchache.
“Nilikuwa
nikijihusisha zaidi na kampuni za kutengeneza filamu, na muziki, matangazo na
hata matamasha au mikutano ya viongozi mbalimbali,” anaelezea na kusema kwamba aliweza kutengenza video za wasanii
mbalimbali, akiwa na kampuni ya Visual Rab chini ya Adam Juma.
Anasema kwa
kipindi hicho, pia alikuwa akifanya kazi kama mwongozaji wa filamu, ambapo
alikuwa akisaidiana na Adam Kuambiana na Benjamini Busungi katika miongoni mwa
kazi zake za filamu.
“Niliweza
kupata uzoefu kwakuwa nilikuwa nafanya kazi nyingi na watu na watu wenye
uzoefu, kiasi cha kuweza kujifunza vitu vingi zaidi anasema.
Baada ya
kupata uzoefu ndipo alipojikita zaidi katika kuhariri picha za video za muziki,
na filamu.
Kwakuwa alikuwa akifanya kazi nyingi, kwa kipindi hicho akiwa chini ya makampuni ya
watu, ndipo alipoamua kufanya kitu kingine tofauti.
Anasema
aliamua kuanzisha tamasha la Bongo Poem, kwaajili ya kusaidia vijana ambao
walikosa nafasi ya kuingia studio huku wakiwa na uwezo mkubwa wa kuimba.
“Wakati
nafanya kazi katika makamkpuni ya watu, watu wengi walinijia na kusema wanaweza
kuimba hivyo wakahitaji zaidi mchangao wangu.”
Kutoka na
hali hiyo ndipo akaamua kuanzisha tamasha hilo, ambalo lengo lake lilikuwa
kuzunguka baadhi ya mikoa ya Tanzania, ili kupata vipaji vipya vya muziki na
kuvisaidia.
Anasema
wakati akiwa katika matamasha hayo, ambayo alianza nayo Dar es salaam, na mikoa
ya jilani ndipo akapata tenda ya kufanya moja ya video ya vikao vya siasa
kilichofanyika Msasani.
Wakati
akiwahi kufunga mitambo ‘Project’ kwa ajili ya kuweza kupata matukio, ndipo
njiani akakutana na foleni kubwa.
Kutokana na
foleni hiyo, ndipo akaamua kushuka kwenye gari lake na kutafuta pikipiki ili
kuweza kuwahi.
Lakini jambo
ambalo anasema bila ya kutegemea ndipo akapata ajali mbaya,2009 maeneo ya darajani Mbezi kwa Komba na
kumsababishia kuvunjika mguu, ambapo alikimbizwa hospitali kuwekewa vyuma
kwenye mguu wake.
Slim anasema
akiwa nyumbani na vyuma vyake mguuni, ndipo vijana wengi waliokuja kumtembelea
wakamshauri kwamba ajiingine kwenye filamu kwakuwa hatoweza tena kuzunguka na
kamera.
Anasema
jambo hilo alianza kulifikiria mara mbilimbili, na kwakuwa alikuwa kitandani
kwa muda mrefu ndipo wazo lakujikita kwenye filamu likaja.
“Nilikuwa
najiuliza kwamba nitaweza kusimama kwa muda mrefu na kamera wakati vyuma vipo
mguuni? Hapo ndipo nikaona ni bora nijikite kwenye kuigiza,” anasema.
Kwakuwa
tayari alishafanya kazi na wasanii wakubwa, na alikuwa akiongoza baadhi ya
filamu kama vile mchukuaji picha ‘Video Camera’ anasema alikuwa na upeo ingawa
si mkubwa sana.
Baada ya
kuanza kupona ndipo alipoamua kujikita kwenye filamu akianza na kuigiza filamu
ya My Angel, ambapo alikutana na wakongwe kama Mlela na Hemedi.
“Baada ya
kufanya vizuri kwenye filamu hiyo, ndipo sasa nikajikubali kwamba naweza kukaa
hapo na kuendelea kufanya vizuri zaidi” anasema.
Anasema
kadri ya kazi zake zilivyokuwa zikitoka ndipo alipozidi kupata mwaliko wa
kafanya kzi nyingine zaidi kutoka kwenye makampuni za watu.
“Nilianza
kupata kazi za kuigiza nyingi, mpaka nikawa nachagua zingine
Kwakuwa
nisingeweza kuzifanya zote” anasema.
Baada ya
hapo sasa akaanza kujikita katika kutengeneza matangazo ya bidhaa mbalimbali,
ikiwemo Bel lager kwa Kenya na Uganda na hapa Tanzania alifanya zaidi ya Kumi.
Anasema pia
amekuwa akifanya matangazo mbalimbali, kama ya Voda com, Tigo, Tulizana, na
matangazo ya kampuni ya soko la hisa la Dar Es Salaam.
Anasema kwa
sasa ameteuliwa kuwa balozi wa benki moja ,
ambayo kwa sasa inaitwa Commercial Bank, pia ni balozi wa nguo za kimarekani
ambazo zinazuia kuharibika kwa ngozi kwa wageni, ambao wamekuwa wakisumbuliwa
na jua.
“Baada ya
kufanya mitindo wa mavazi yanayotengenezwa na Wamarekani, kwaajili ya kujilinda
na jua ndipo wakaamua kunipa na ubalozi” anaelezea.
Kwa sasa
malengo yake anasema kumalizia filamu yake ya Coast To Coast ambayo itakuwa
filamu ya kwanza kutengenezwa mwaka nzima, na kuchukua wasanii wa nchi mbalimbali.
Anasema
filamu hiyo tayari imekutanisha wakari kutoka ujerumani, kama Van, Clara na
Maria, Tanzania ni Batuli, Wastara Juma, Adam Kuambuana, Ben, Jamse, Tito,
Muogo Mchungu, yeye mwenye na Mkenye mmoja.
Huyo ndio
Slim Omari, ambaye ni mzaliwa wa Dar es
salaam, baba yake mzee Omari alikuwa mtu
wa Yemen lakini mama yake ni mswahili.
Shule ya
msingi aesomea Temeke Magede, na kujiunga na Elimu ya sekondari ya Saba Saba
International, na baada ya hapo akaendelea na kujiendeleza na masomo mengine.
Mwisho.


No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi