Saturday, November 23, 2013

Kama unaweza kusugua gaga@Subiri bingo la Shaa

Kama unajijua wewe ni mkali katika suala zima la kudensi, hasa kudenzi nyimbo za uswahili, basi sikiliza hii. Nyota wa muziki wa kizazi kipya, kwa sasa anayefanya vizuri na kibao cha Sugua Gaga, Sarah Kais 'Shaa' amesema anahitaji kutafuta wacheza shoo, kwaajili ya matamasha yake yanayokuja.

Hivyo kama unajijua wewe ni mtaalamu hasa wa kusakata rhumba la uswahilini, basi fuatilia hapa ili kujua ni wapi na lini atahitaji watu hao kwaajili ya kufanya usahili na kujiunga moja kwa moja na kuwa densa wake wa kudumu.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi