Mnaweza wote kuwa waigizaji kati ya Baba na Mwana, lakini
filamu ambzo mkaigiza wote pamoja zikawa chache au zisiwepo kabisa. Hawa ni miongoni mwa wasanii walioigiza filamu moja na
watoto wao, Will Smith katika filamu After Earth na mwanaye Jaden Smith ambaye
tayari alishang’aa katika Karete Kid na Jack Chan.

Robert Downey Jr
ambaye aliigiza kama Irone Man 1,2,3 pia akaigiza katika filamu ya
Avenger, naye aliigiza na baba yake anayeitwa Robert Downey Sr, ambaye ni
mwandishi na Director ambaye maarufu kwa kutengeneza na kubana bajeti katika
filamu zake katika miaka ya1960 na 1970. Ambapo waliigiza katika filamu ya
Pound, baba Sr aliigiza kama kijana mwenye umri wa miaka 18,
aliyekuwa akifuga mbwa na baadaye kumuokota mtoto ambaye ndiyo Jr (Mwanaye).
James Caan yeye alishawahi kuigiza na baba yake, Scott Caan
mara mbili. Walicheza
kwenye filamu ya 'A boy Called Hate mwaka 1995 na katika filamu Mercy mwaka
2009.
Ninapomzungumzia
Josh Brolin
nadhani utamkumbuka zaidi katika filamu ya MIB (Men In Black) ambayo yupo Will
Smith, nadhani umeshamkumbuka yule babu mwenye vituko.
Yeye
na baba yake James, walikuwa kwenye filamu ya My Brother War, huku baba mtu
akiigiza kama kiongozi wa mgogoro na mwanaye aliyeigiza kama ndugu yake
akimsindikiza katika vita hivyo.



No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi