Naweza
kusema kwa sasa soko la filamu limetanua, ingawa zipo baadhi ya filamu hizo zipo zenye ubora
wa kuridhisha na baadhi yake zimeendelea
kuwa tatizo kutokana na mpangilio mbovu wa filamu zenyewe au stori.
Hilo sio
tatizo sana ila kubwa zaidi ni katika suala la utumiaji wa majina ya filamu
mengi yao kuwa ya lugha za kiengereza, ambapo ndipo ilizaa makala hii.
Majina mengi yamekuwa yakija kwa mtindo wa
Lugha ya Kiengereza, husasani filamu zinazotoka hivi karibuni zikiwemo
Imposible, God Promise, Ghost Calamities na nyingine kibao, Before Wedding,
Apple na zingine nyingi.
Kabla sijaanza
kuulizia zaidi chanzo cha kuingia kwa majina ya kiingereza kwenye tasnia ya
soko la filamu Tanzania, nilijaribu kudadisi ni nani wa kwanza kutumia jina la
filamu la kiengereza.
Lakini
baadhi ya wadau wa tasnia hiyo, ambao ni wateja wa kasi hiyo ya sanaa wengi
walisema kwamba, kuibuka kwa nguli wa tasnia hiyo marehemu Steven Kanumba na
swahiba wake wa karibu Vicent Kigosi ndiyo mwanzo wa kuibuka kwa filamu za
lugha ya kigeni.
Mmoja wa
Watanzamaji wazuri wa filamu za kitanzania, ambaye jina lake hakutaka litajwe,
alisema Kanumba alifanya hivyo kutokana na kuwa na malengo ya mbali na filamu
zake, na ndiyo maana alifanikiwa kufikisha soko la filamu zake mbali.
Alizitaja
baadhi ya filamu ambazo alifanya marehemu Steven Kanumba, ambazo zilitumia
majina ya kiengereza ni kama Off Side, Uncle JJ, This Is It na zingine kibao.
Lakini hata
hivyo swahiba wake Vicent Kigosi ‘Ray’ naye alikuja na filamu kama, Family
Diserty, Hot Friday, I hate My Birthday, Danger Zone na nyingine kibao.
Hata hivyo
utumiaji wa lugha hiyo katika filamu za kitanzania, wasanii wenyewe wamekuwa na
mtanzamo tofauti tofauti, na baadhi ya wasanii na wadau wa tasnia hiyo
walieleza mitazamo yao.
Nyota wa
filamu nchini, ambaye alishatengeneza filamu kama Tifu la Mwaka, Shahaada,
Toba, Fungate, Suria, Issa Musa ‘Cloud 112’, yeye alisema anaona ni kama
ulimbukeni wa kutumia lugha za kigeni.
Ingawa
anaona huenda mtu akawa anafanya hivyo kutokana na maslahi yake binafsi.
Cloud 11
anasema yeye ataendelea kutumia majina ya lugha ya Kiswahili, katika kuhakikisha
anaendeleza utamaduni wa lugha hiyo.
Lakini
mwigizaji nguli, ambaye aliibuka na filamu kama Miss Bongo, Kijogoo, Sweat Lie,
huku akishirikisha katika filamu kama Red Card, Sobbing Sound, Haji Adam ‘Baba
Haji’.
Baba Haji
ambaye ni muhitimu wa sanaa ya filamu ya jukwaani, anasema kutumia lugha ya kiengeleza au ya
kigeni ni kulenga soko la kimataifa.
Anasema hata
hivyo ni vizuri watu wanaotumia lugha ya kiengereza au ya kigeni yoyote, kuweka
na tafsiri ya jina la filamu hiyo.
“Ni bora
kutumia lugha ya kigeni na kutafsiri Kiswahili kwaajili ya soko la ndani” anasema.
Anasema siku
moja wakati yupo kwenye kazi zake za uigizaji nchini Zambia, alikuwa
akilalamikiwa kwamba kila kitu Kiswahili, jambo amblo wengine wanazipenda
filamu lakini wanashindwa kuzielewa.
“Lakini pia
tunapotumia kutafsiri filamu , tuna mpa
mtu kazi ya
kufuatilia
filamu, na kufuatilia mikasa” alisema.
WWakati huo
mmiliki wa kampuni ya Bulls, inayojihusisha kutengeneza filamu nyingi za hapa
nchini, pia mwongozaji wa filamu mbalimbali, Single Mtambalike.
Anasema
katika filamu zake zote, filamu ambazo ametumia lugha ya kiengeleza ni mbili,
Gent Men, na The Stranger, lakini zilizobaki zote ametumia majina ya Kiswahili,
kama Uyoga, Swahiba ,Chaguo Langu ,Tamaa Yangu,Jesica ,Mtaani Kwetu ,Kimya .
Anasema yeye
huwa analenga sana soko la Tanzania hususani kwa watu wa mitaani, ambao elimu
yao haipaswi kuhakikiwa sana kwa lugha ya kigeni.
“Kama filamu
zangu nategemea kwanza soko la ndani, sioni sababu ya kutumia lugha ya kigeni”
alisema.
Anasema huwa
anatumia lugha ya kiengeleza kama kutafsiri, yale yanayosemwa ndani ya filamu
lakini jina la filamu linabaki kuwa la Kiswahili.
Kwanza
alieleza wazi dhumuni la shirikisho, ambalo ndilo lenye mamlaka ya kusimamia
kazi za wasanii wote Tanzania.
Anasema
lengo la shirikisho kupambana na maadili, ikiwemo utumiaji wa lugha, mavazi na
mambo mengine.
Hata hivyo
anasema hali hiyo imekuwa kazi ngumu kutekelezeka kutokana na shirikisho
kuandamwana na mambo mengi ya kufanya.
Kwa upande
wa kampuni yake anasema kutumia lugha ya Kiengereza katika filamu zetu,
kunatokana na soko la ndani lenyewe kuhitaji hivyo.
Miongoni mwa
wasanii ambaye naye alitoa maoni yake ni, mwigizaji aliyewahi kuwa
mwanamitindo, Yusufu Mlela ambaye tayari alishatoa filamu zake kama Angel, Poor
Mind.
Kwa upande
wake anasema kufanya filamu za Kiswahili na kuweka jina la Kiengereza, ni kukuza soko la kimataifa.
“Ni vizuri
kutumia Kiengereza, lakini chini kutafsiri Kiswahili ndiyo inapendeza zaidi”
anasema.
Anasema
kwasasa watu wanalenga zaidi soko la nje, ambapo watu wengi hawajui Kiswahili.
Hivyo wanatumia lugha ya kigeni, ili kuwavutia watu ambao hawajui Kiswahili.
Msanii wa
kike, ambaye kwasasa huenda ndiyo akawa msanii pekee wa kike aliyeigiza filamu
nyingi, Chuchu Hansi aliyetengeneza filamu ya Two Face, na Laura.
Anasema
filamu ya Kiswahili kuweka jina la kiengeleza, kunatokana na stori yenyewe ya
filamu.
Anasema hata
hivyo kutoka moyoni kwake anatamani sana filamu kuwa na majina ya Kiswahili,
ili kukuza lugha yetu.
“Tusiwe
dhaifu sana katika hilo, Kiswahili
kimekamilika ni bora kutumia zaidi lugha yetu” anasema.
Miongoni mwa
wadau wa filamu waliotoa maoni yao, ili kujua ni vema kuendelea kutumia majina
ya Kiengereza katika filamu za Kiswahili, ni Makamu mwenyekiti wa chama cha
wasambazaji wa filamu Tanzania, pia ni Pia ni mkurugenzi wa Bajomba Film
Distibuters, na mjombe wa shirikisho la filamu Tanzania ‘TAFF’ Makame Juma
Bajomba.
Bajomba
anasema hata katika maisha ya kawaida, Watanzania wenyewe, wanapenda
kuchanganya lugha ya kiengeleza na Kiswahili.(Pata utamu zaidi)
“Ujue
ukitumia lugha ya kiengeleza, watu wanataka kujua linamaana gani zaidi. Hivyo
watu wanajikuta wakinunua ili kuweza kujua zaidi” anasema.
Anasema hata
hivyo lazima wasanii waamke na kutumia lugha za asili, katika kukamilisha
filamu za Tanzani, ili kuweza kuwavutia wageni.
“Mbona kuna
filamu kama Gawa au Odama, zimefanya vizuri tena zimetumia lugha ya kiasili”
anasema.
Mwandishi wa
gazeti la Habari leo, na Mchambuzi wa filamu Beda Msimbe, yeye alifafanua zaidi
kwa kusema.
Jina huwa si
tatizo sana kwenye filamu, kutokana na jina sio hali harisi ya filamu yenyewe.
Anasema
utumia jina la kigeni, ni sahihi kwakuwa hata nchi zilizoendelea pia hutumia
lugha ambazo zisizozilizomo ndani ya filamu yenyewe.
“Zipo filamu
nyingi ambazo majina yake sio kilichopo ndani, wala hayaendani na lugha ya nchi
husika” anafafanua.
Akitolea
mfano wa filamu kama Matrix ambayo asili yake ni mahesabu, lakini filamu
haihusiani na mahesabu kabisa.
Aliendelea
kutaja baadhi ya filamu, ikiwemo Terminater, na zingine ambazo hutumia majina
ambayo hayaakisi picha yenyewe.
“Cha msingi
watu huangalia soko, na sio kuangalia jina lina asili ya wapi, na linamaana
gani” anaendelea kufafanua.
Mwisho.




No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi