Huenda ukawa
hujui, lakini ndivyo ilivyo nyota wa ngumi Tanzania na Afrika Mashariki na kati
Pendo Njau, ameamua kukimbilia katika uigizaji wa filamu baada ya kushindwa
kuvumilia rushwa ya ngono iliyokuwa ikimwandama.
Hayo
yalijitokeza baada ya kuhitajika kwenda katika pambano la K One, ambalo ni
miongoni mwa mapambano makubwa yanayofanyika Japan, huku zikihusisha nchi
tofauti za duniani.
Si nafasi
ambayo kila mtu anaweza kuipata, lakini nguvu akili na ujasiri wa kushinda
mapambano ya kimataifa ndiyo unafanya kutumiwa barua na uongozi wa ligi hiyo.
Hayo na
mengine mengi, ndiyo yaliyomfanya mwandishi wa makala hii, kumtafuta na kutaka
kujuzwa na kudadavuliwa zaidi.
Anajulikana
zaidi kwa jina la Pendo Njau lakini mwenyewe,
anasema hilo jina lake lakini jina harisi alilobatizwa nalo ni Hellena Honest
Njau, anasimulia na kusema matatizo yote yalianza baada ya pambano la mwaka
20011.
Pambano
hilo alipambana mpiganaji wa Kick Boxer
kutoka nchini Kenya Rukia Nachirite, na kufanikiwa kuchukuwa ushindi wa Afrika
Mashariki na kati.
Ushindi huo
anasema uliweza kumwongezea umaarufu mkubwa, kwa wapiganaji wa kike wa Afrika na duniani kote kutokana namchezo wa ngumi.
“Niliweza
kujulikana kiasi cha kuanza kupata mwaliko, kwa mabondi kutoka Afrika Kusini” anasema.
Miongoni mwa
mwaliko ni kutoka kwa mpiganaji wa
Kickboxer, kutoka Afrika Kusini, Farasi
Coat, ambaye pambano hilo lilimpaswa Pendo kutetea mkanda wake wa Afrika
Mashariki na Kati.
Farasi Coat alikuja nchini, alijitahidi ndipo kwa mara ya
pili akafanikiwa kubaki na mkanda, na ndipo ukawa mwanga wa kuchaguliwa kwa
kuletewa barua kutoka Japan.
“Nilitumiwa
barua ya mashindano ya ligi ya K One, yanayofanyika Japan kila mwaka, nikawe
miongoni mwa washiriki wa mapambano hayo” anasema.
Lakini Pendo
anasema hali ilikuwa tofauti pale alipohitajika kuwa na fedha kama 15 au 20,
kuweza kukidhi safari yake hiyo kwa kukaa katika nchi hiyo kwa muda wa mwezi
mmoja na ghalama zingine ndogo ndogo.
“Nilianza
kutafuta fedha lakini nilishindwa kabisa, kutokana na ushirikiano mdogo wa
kimichezo” aliendelea kusisitiza,
Hapo ndipo
alipoanza kukutana na vituko, baada ya kuamua kwenda kwenye maofisi ambayo
yamekuwa akiamini yanauwezo wa kumdhamini.
Anasema
wengi wakajitokeza kuanza kumwekea ahadi ya kumchangia kwaajili ya safari hiyo
ambayo ilianza kuonyesha nuru ya mafanikio katika mchezo wa ngumi kwa upande wa
Wanawake Tanzania.
Ulifika muda
wa kufuatilia ahadi, anasema hapo ndipo vituko vilipoanza kwa kuitwa kwenye
hoteli kubwa na kuwekewa mitego.
“Mtu ulikuwa unamheshimu, anakupigia simu
uende kwenye hoteli ili akakupe hizo
fedha, tena anakwambia yupo kwenye
kikao. (Endelea kusoma ujue cha zaidi)
Lakini
ukifika huko, anakuambiwa njoo kwenye chumba namba fulani. Na ukienda unamkuta
na taulo, na kukuambia kama unataka fedha ulale naye kwanza’Ufanye mapenzi’ ”
anasema Pendo.
Ukikataa
anakuruhusu uondoke bila ya kukupa saidia chochote, jambo ambalo lilizidi kumkatisha
tamaa.
Anasema kila
alipojaribu kwenda kuomba masaada kwaajili ya kusafiri, lakini ilishindikana
kwakuwa tabia ilikuwa ile ile ya kumuhitaji kimapenzi kwanza, harafu msaada
baadaye.
“Nikaona
siwezi kukubali kuchezewa, ndipo nikaghaili hiyo safari na kuamua
kujishughulisha katika masuala mengine madogo madogo” aliendelea kusema.
Lakini hata
hivyo mwaka 2012, alitumiwa barua nyingine katika mashindano hayo. Ndipo
akaamua kufanya kazi kama promota au mwaandaaji wa mapambano ili kuweza
kukusanya fedha kwaajili ya safari.
Miongoni mwa
mapambano ambayo aliyaandaa ni ya Kasema na Oswad Maneno, ambalo la kwanza
Kaseba alishinda lakini mpinzani wake alikataa.
Pia akaandaa
pambano la marudiano, kati ya mahasimu hao wawili. Lakini baadaye tena akaja
kuandaa pambano la Rasikosi Mwanza wa Malawi, ambapo alipigwa katika raundi ya
tano lakini mapambano yote hayo hakuweza kufikia fedha iliyohitajika na hatmaye
akabaki tena bila ya kwenda popote.
“Sasa
niliona mchezo wa ngumi hauna faida kwangu, kwakuwa nimeambualia umaarufu”
anasema
Anasema
tangu aliapoanza ngumi mwaka 2002, hakuna mafanikio yeyote aliyoyapata.
Pendo
anasema histori yake ya kupigana ilianzia shule ya msingi hadi sekondari, kwa
kupigana na vijana wa kiume kiasi cha kuanz kumuogopa.
“Nilikuwa nikipigana na mwanaume, nilikuwa
nakunja ngumi na kama mzembe mzembe alikuwa lazima nimwangushe. Watu niliokuwa
nasoma nao walivyosikia nimekuwa mpiganaji hawakushangaa” anasema.
Anasema
kipindi hicho alikuwa akisoma shule ya msingi Olong’adida iliyopo Manyara,
ambapo baadaye akafauru katika shule ya sekondari ya Gallapo day iliyopo
Manyara hapo hapo.
Baada ya hapo
alianza kutafuta maisha, hadi kufikia kuja Dar es salaam kwa ndugu zake na
kuwaacha wazazi wake mkoani Manyara.
“Sisi ni
watu wa Moshi, lakini kama unavyotujua wachaga tunahama mikoa kwaajili ya
kutafauta fedha” alisema.
Baada ya
kufika Dar es salaam ndipo aliapoanza kuweka nia yake ya wazi kutaka kujiunga
na mchezo wa ngumi, ambapo rafiki zake wa karibu waliweza kumfikisha hadi kwa
Japhet Kaseba, bigwa wa mchezo wa Kick Boxer dunia.
Mwaka 2002
alianza rasmi mazoezi, katika pwani ya Coco Beach akiwa na mpiganaji Kaseba, na
baadaye akaanza kupigana katika mazoezi.
“Lakini
baadaye Kaseba alikuwa anasafiri, ikabidi anikabidhi kwa Master Kinyogori”
anasema Pendo.
Wakati
alipofika kwa mwalimu huyo wa ngumi ya Boxer, alianza kujifunza boxer. Anasema
mwalimu huyo kwanza alimuona kama msichana mrembo, lakini alipoanza kumjaribu na wanaume ndipo
aliposhituka akiwapiga.
“Alianza
kuniamini baada ya kuwadondosha wanaume ambao yeye alikuwa akiwaamini’ anasema.
Ndipo
nikaanza mazioezi rasmi kama KickBoxer, ambapo mwaka 2008 nikapigana pambano
langu la kwanza na Rehema Chande.
“Niliweza
kushinda kwa pambano langu la kwanza, jambo ambalo lilinifanya kuchukua mkanda
w mpiganaji bora wa Tanzania” anasema.
Aliweza
kushinda pambano hilo kwenye raundi ya 5, akiwa na point 3 na kufanikiwa
kuchukua mkanda wa ngumu wa Tanzania upande wa wanawake.
Anasema
mkanda huo ulitolewa na chama cha ngumi cha Ufaransa, kilichokuwa kikiitwa
World Kickboxer Network (WKN).
Baada ya
hapo akaja kupigana tena katika pambano la Boxer, na Flora Malichela, mwaka
2009 Octoba ambapo napo alishinda.
Baada ya
hapo ndipo nikapata pambano la kupigana na Rukia Machirite, kutoka Kenya katika
ubigwa wa Afrika Mashariki na kati, ambapo ulikuwa mwaka 2011.
“Pambano
hilo nilifanikiwa kushinda na kuapewa barua ya kwende kwenye mapambano ya K
One, Japani” anasema.
Baada ya
kutopata maendeleo yoyote, ndipo mfanyabiashara Dotnata Posh, aliamua
kumchukuwa na kumuingiza kwenye filamu.
“Napenda
sana kumshukuru Dotnata, ambaye alinishauri niachane na ngumi na baadaye kunipa
nafasi katika filamu” anasema.
Anasema kwa
sasa anashafanya filamu ya Bongo Mafia, ambayo ameigiza na wakali wengi wa
mchezo wa ngumi, kama Japhat Kaseba na Mchumia Tumbo.
“Nimeweza
kuwa na fikra mpya, baada ya zamani kushindwa sasa hivi lengo lipo kwenye
filamu’ anasendelea kusisitiza.
Anasema
kutokana na kila sehemu kujaa ngono, hivi sasa ameamua kujipatia ridhiki kwa
kuwafundisha wakina mama, ambao wameshindwa kwenda kwenye mazoezi na kuomba
wafundishwe nyumbani kwao.
Anasema huwa
analipwa fedha kwa kuwafundisha mazoezi, au kuarikwa kwenye Gym, kwaajili ya
kuwafundisha watu.
“Kwasasa
sina uwezo wa kuanzisha Gym, langu ila ningepata uwezo hata watu wa kunikopesa
basi ningefungua na kumlipa kutokana na kile kiingilio” anaelezea.
Pendo ni
mtoto wa tatu, kati ya watoto nane ambapo
mkubwa wao ameshafariki.
Kwa mara ya
kwanza wazazi wake waliposikia anacheza mchezo wa ngumi, walimuonya kuwa makini
lakini hawakuweza kumzuia sababu tayari walishaona dalili tangu mwanzo.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi