Huenda
ukajiuliza kwanini muziki wa Tanzania,
hususani muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva, ambao umeanza katika
miaka ya tisini, lakini umeendelea kusuasua
katika ukuaji wake katika soko la kimataifa.
Mara nyingi
wapenzi , wadau na wanamuziki wenyewe wamekuwa wakiulizana mchawi ni nani? Na wengine kushikana uchawi wenyewe kwa wenyewe.
Lakini bado
wakibaki na swali ni nani anazuia muziki
huu usifike mbali, na kubaki kudumaa
katika nchi za Afrika Mashariki, huku
wasanii wake wakipata umaarufu na fedha za muda mchache na baadaye kupotea kama moshi wa sigara.
Hivi
karibuni mwandishi wa makala hii, kwa
bahati alifanikiwa kuiona moja ya video
ya Tanzania inayoitwa Jikubali, iliyoimbwa na msanii Ben Poul, ikionyeshwa
kwenye moja ya luninga yenye nguvu kubwa Afrika na duniani yenye
makazi yake huko Afrika Kusini ya inayoitwa
Channel O.
Hapo ndipo nilipoamua
kumtafuta msanii huyo na kumuuliza, njia gani aliitumia na kufanikiwa kupenya hadi wimbo wake kufika huko. Pia
kutaka kujua ni kwanini wasanii wengi
wanashindwa kufikia hapo alipofikia yeye, inagawa wamekuwa wakifanya kazi nzuri
na kujipatia umaarufu mkubwa.
Ingawa kwa
mara ya kwanza mnamo miaka ya 2000, video ya mwanamuziki Judithi Wambura ‘Lady Jay Dee’ wimbo uliobeba
albamu yake ya kwanza ‘Machozi’ uliwezwa kuonyesha.
Katika mika
hiyo hiyo Kharid Mohamed ‘T.I.D’ na wimbo wake wa Tanzania Mie nao ukafanikiwa
kutamba katika kituo hicho, hata hivyo
kwa muda wote huo hadi leo hii video
bado zimekuwa zikisuasua kusogea mbele.
Ben Poul
alianza kusema kwamba video yake, tofauti na video zingine ambazo zimekuwa
zikipigwa katika kituo hicho cha luninga, ambazo zimekuwa zikighalimu zaidi ya
milioni 10.
Anasema
video hiyo, imemghalimu milioni 5 kuikamilisha lakini pia zilikuwa zikimtoka
fedha zingine ndogo ndogo ambazo zilikuwa hazipo kwenye mahesabu.
“Kikubwa sio ghalama kubwa ya kufanya video
ndiyo ikaonyeshwa kamataifa, ila uzuri wa video na mazingira” anasema.
Anasema
video yake aliifanya mkoani Arusha, chini ya mtayarishaji Nisher, ambaye kwa
sasa anakuja kwa kasi.
Ban Poul
anasema kabla ya kufanya video hiyo, alihakikisha anakamilisha kila kitu ilikuona
anajituliza juu ya kazi yake.
Baada ya kuhakikisha
amemaliza kazi zake zote, akahamishia nguvu zake kwenye video hiyo ambayo
ilichukuwa wiki moja na nusu, kuikamilisha.
“Video
inahitaji utulizaji wa akili, sio mtu unataka umalize kwa siku mbili, au tatu
ili kukimbia bajeti. Pia mtayarishaji
sio anakuwa na haraka amalize ya kwako siku bili, akafanye ya mwingine, wote
mnabidi mtulie” anasema.
Anasema
katika video nzima ameonekana peke yake, ingawa ndani ya wimbo wenyewe alitaja
majina ya wasanii, wanasiasa, na watu wengine zidi ya majina ishirini.
Lakini
kutokana na mpangilio wa video hiyo, hakupaswa kuonekana mtu yoyote hata kwa
bahati mbaya.
Walitumia
wiki moja na nusu kuhakikisha wanapata picha za uhakika, na zenye mvuto na
ndipo ikapatikana video hiyo ambayo ilianza kutikisa hapa nchini.
“Video ikawa
imekamilika kwa mtindo huo, sikuwa na mtu yoyote katika video hiyo ambaye
ningesema nilikuwa nae” anasema.
Kuhusiana na
video yake kupigwa kwenye luninga ya Channel O, anasema kwa mara ya kwanza alishawahi kupeleka video
zake kwa mawakala wa Mtv Base na Channel O, waliokuwepo hapa nchini.
Video
alizopeleka ilikuwa Maneno Maneno, na Samboila, lakini hazikuweza kufanya
vizuri katika mchujo wa kuonyeshwa katika luninga hizo.
Lakini
hakukata tamaa, alihakikisha kila siku anajitahidi kufanya vitu vingine zaidi
mpaka akafanikiwa kwa video yake ya
jikubali kuonyeshwa.
Hata hivyo
anasema kinachopelekea video za Kitanzania, kuwa nyuma, ukitofautisha za Kenya,
Ghana na Nigeria katika kuonyeshwa
kwenye luninga hizo, ni kutokuwepo kwa ushirikiano kwa wasanii wa Tanzania.
“Kila mtu
anapanda kimafanikio kivyake, hakuna mtu ambaye anaweza kufanikiwa kwa kupitia
mgongo wa mwenziwe. Lakini wanasahau hata kusaidiana” anasema.
Huenda hilo
ndilo likawa tatizo kubwa, maana kila mtu anaanza hatua moja na sio mtu
kuendeleza hatua ambazo mwenzake ameziacha.
Ben Poul
anasema ukimfuata msanii mkubwa ambaye tayari video yake moja au mbili
ilishaonyeshwa kwenye luninga hizo maarufu Afrika na Duniani, atakujibu kwamba
video yake imeghalimu fedha nyingi sana kutengeneza, au anaweza kukujibu kwamba amehonga ili
kuicheza.
“Mtu
ukimfuata kumuuliza juu ya kufanya vizuri kwa video yake, kwa lengo la
kujifunza kupitia kwake anaweza kukukatisha tamaa kabisa” anasema.
Anasema hali
hiyo imepelekea kuleta ugumu katika kuuliza, kwa maana hutopata jibu la
uhakika. Hivyo anasema wasanii wengi wamekuwa wakianza hatua moja, na kila
anayekuja amekuwa akianza hatua moja tena na wengi huishia njiani.
“Ilibidi
hatua moja atakayovuka mmoja mwingine apate ushauri kutoka kwa yule, na hata
kujua njia alizotumia ili asije akaanza mwanzo” anasema.
Anasema hadi
video yake inafika pale ambapo imefika sasa hivi, ni juhudi zake mwenyewe bila
ya kupata ushauri wowote zaidi ya kutuliza kichwa na kufanya kazi nzuri.
Lakini
anasema kama kungekuwa na elimu nzuri, au ushirikiano baina ya wasanii wenyewe
basi wasanii wengi wangeweza kufikisha mbali video zao.
Hiyo ndiyo
miongoni mwa sababu kubwa ya kutosogea, au kusogea kwa kusua sua kwa muziki wa
kizazi kipya katika soko la kimataifa ingawa, baadhi ya nyimbo zimekuwa
zikifanya vizuri.
Miongoni mwa
msanii ambaye niliwahi kumuuliza ni Emmanuel Rlibariki, ambaye yeye alisema
wasanii hawapendani.
Anasema
hawataki kumuona mtu anafanikiwa, hasa kupitia yeye anahitaji kila mtu
kupambana mwenyewe.
“Mtu hataki
kumuona msanii mwenzake anafanikiwa, wala kula chachu ya mafanikio ya mwenzake”
anasema.
Huenda
wasanii wasanii wengi wamesahau kwamba umoja ni nguvu, na utengano wao ndiyo
sababu ya kuumia kwao kimaslahi na hata kimuziki kiasi cha kuonyeshana kidole,
kumtamtafuta mchawi.
Mwisho.



No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi