Doreen alionesha utofauti kwa
kupitia mbele ya majaji akiwa na wanamitindo wa aina mbili ambapo mwanzo
walietembea wanamitindo wa shoo hiyo na baadae aliwatumia wanamitindo wa kwake.
Akizungumzia hatua alisema
kuwa kwa kuwa ujumbe alionao mwaka huu ni Revolution akiwa na maana ya
mabadiliko ambapo amesisitizia zaidi suala la mabadiliko ya fikra.
Alisema kuwa hiyo ndio sababu
ya kuwatumia wanamitindo wengine ambao wao wameonesha ni ya kuleta mabadiliko
nchini kwa kujikita kufanya kazi ambazo zimekuwa zikionekana kuwa ni za watu wa
sirika fulani.
Kwa upande wa mavazi yake
aliyoyabuni Doreen ameonesha mavazi ya aina mbalimbali ambapo asilimia kubwa
yalikuwa yakionesha utupu.
Akzungumzia hilo alisema kuwa
mavazi aliyobuni kwa onesho la Swahili Fashion mwaka huu yamejumuisha aina
mbili ya ngu ambapo moja inaonesha uwazi lakini ya pili inakuwa inafunika kwa
ndani.
“ Najua nimetaka kuonesha
utofauti kidogo kwa mwaka huu ambapo mavazi haya ni mazuri na yanafaa zaidi
wakati wa joto, mimi nimesisitiza zaidi suala la mabadiliko ya fikra ikiwa ndio
ujumbe wangu kwa mwaka huu” alisema Doreen.
Onesho la Swahili Fashion kwa
mwaka huu yameoshirikisha wabunifu mbalimbali kutoka nje ya nchi huku wabunifu
wa ndani wakiwa wengi pia na wamewakilisha vema.
Mwisho
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi