NYOTA wa
filamu nchini ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa mweka hazina wa Bongo Movie, Single Mtambalike ‘Richie
rich’ amesema filamu yake ya Uyoga tayari ameshaingiza sokoni na anategemea kuleta
makubwa juu ya filamu hiyo.
Richie
alisema tasnia imetanuka sana, hivyo
kila mtu amekuwa macho kuangalia kazi yake iwe nzuri na sio kutegemea jina kama
zamani.
Alisema
katika filamu hiyo, ambayo imemkutananisha tena na Vyonne Charry ‘Monalisa’, ambaye
alitokana naye kundi moja la Nyota
Ensemble ‘Mambohayo’, ambaye humo
ameshiriakiane naye vizuri sana.
“Ni filamu
ambayo nimetumia akili nyingi na kwa muda mrefu, maana ni filamu ipo tofauti
sana kuliko filamu zangu zingine” alisema.
Alisema
filamu hiyo imeingia sokoni, hivi karibu kwahiyo anatarajia kufanya makubwa
zaidi kupitia filamu hiyo.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi