MWIGIZAJI nyota
wa filamu nchini Vicent Kigosi ‘Ray’, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa
Bongo Movie, baada ya kushinda kwa kura 53 kati ya 54 huku akiahidi kupambana
na waandishi wanaowadhalilisha wasanii wa filamu.
Akizungumza
katika kikao baada ya kushinda kiti
hicho, alisema hatofumbia macho
waandishi wanaojaribu kupotosha ukweli juu ya mambo mbalimbali
yanayowahusu wasanii wao.
Pia
aliendelea kwa kusema atapambana na wasanii ambao wamekuwa chanzo cha kuvuja
siri za ndani kabisa za wasanii wenzao kwa kwenda kuuza stori kwa waandishi.
“Tunawajua
wanaokwenda kupeleka stori kwa waandishi na kuwachafua wenzao, lakini safari
hii hatutokubaliana nao” alisema.
Ray alisisitiza
kupambana na mahojiano ya uchochezi kwa mtu kuhojiwa upande wa kwanza na upande
wa pili kuhojiwa mwenzake na kuwatengenezea bifu bila kujijua.
Miongoni mwa
wasanii wengine waliochaguliwa katika kamati hiyo, ni Jackline wolper, Irene
Uwoya, Single Mtambalike.
Wakati huo
msanii Jacob Stephan, yeye ndiyo aliyekuwa akimalizia muda wake na kumwachia
Ray, kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mwingine.
Huu ndiyo uongozi mpya wa Bongo Movie, Jack Wolper, Vicent Kigosi, Rado, Single Mtambalike, Irene Uwoya na wengine.
Vicent Kigosi mwenyekiti mpya wa Bongo Movie
Jack Wolper mweka azina msaidizi
Richie rich mweka azina wa Bongo Movie
Shemsa Ford akitoa changamoto chake juu ya uongozi ujao
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi