NYOTA wa filamu nchini Wema Sepetu , amesema
kutoonekana kwake kwa watu kunampa furaha na faraja kwakuwa alishachoka kutajwa
tajwa midomoni mwa watu.
Wema
alisema kuulizwa mbona siku hizi haonekani na wasanii wenzake
kuna mpaimani kwamba hapatikani ovyo jambo analohitaji liwe hivyo siku zote.
Alisema kwa sasa kila kitu atakuwa akifanya kwa siri,
kutokana na kuamini umaarufu si kila
kitu chako kiwe wazi kwa wengine, kama ilivyokuwa zamani.
“Nafurahi
sana ninapoambiwa mbona sionekani, na wengine wanaponitafuta na kunikosa”
alisema
Wema alisema
hata safari zake za ndani na nje ya nchi, zote zitakuwa siri, na wala hataki kitu chochote kinachomhusu yeye kuwa
nje.
Aliendelea
kusema hivi sasa atakuwa akifanya kazi zake zote kimya kimya, akiamini huo ndio
umaarufu ambao anautaka na sio wa kuweka wazi mambo hadi ya siri.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi