Mwigizaji ‘Dk Cheni’ amekiri mauzo mabaya ya filamu yake ya My Flower
lilimfanya abadili sokola filamu na kuingia vichekesho. alisema
alikuwa na desturi ya kuulizia kila kazi zake zinazoingia sokoni, lakini
alipoulizia kuhusu kazi hiyokwenye maduka aliambiwa wazi kwamba imedorora.
Alisema
tatizo hilolilimuumiza sana kichwa, mpaka kuamua kuirudia kuingalia mara mbili
mbili hadi alipoamua kubadilika na kuanza kufanya filamu za vichekesho
‘Comedy’.
Miongoni mwa
filamu za vichekesho alizofanya ni Dhuluma, Return Love, Dk wa Kifimbo na
Majanga.
Pia Dr Cheni
alieleza sababu ya wao kushindwa kumudu soko la kimaifa, kunatokana na gharama kuwa kubwa za kuwaita wasanii wa nje wakati kipato chao kipo pale
pale.
Alifafanua
zaidi kwa kusema kwamba wasanii wanatamani kuigiza na wasanii wakubwa kutoka nje kama Nigeria
na Ghana, lakini kutoka na gharama kuwa kubwa za kumleta msanii, hata hivyo
wakipeleka kwa Msambazaji hulipwa fedha zile zile za kawaida.
Dk Cheni alisema
Msambazaji hatizami umetumia kiasi gani katika kazi hiyo, anachojali yeye
kukupa kile kiasi chako hata kama atauza mapato makubwa zaidi.
Alisema
jambo hilo limekuwa likiwakatisha tamaa, na kuona haina haja ya kuingia gharama
kuwaleta wasanii wa nje wakati
wanachopata ni kile kile cha siku zote na kuwafaidisha wengine.
Aliendelea
kwa kusisitiza na kusema , wanachowaingizia wasambazaji ni kikubwa kulikokile wanachopewa na wanashindwa kufanya
lolote sababu wasambazaji wanahaki kubwa.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi