MSANII wa muziki wa
kizazi kipya Barnaba ameungana na mabalozi wengine katika kuhamasisha
ujenzi wa hosteli za wanafunzi wasichana. Barnaba anaunga na
Nancy Sumari, Faraja Kota na Rebeka Giuni katika kampeni hiyo inayolenga
kukusanya bilioni 2.3 na kujenga hosteli 30 ambapo Barnaba atashiriki
matembezi hayo.
MAMLAKA ya
Elimu Tanzania (TEA) imeandaa matembezi ya hisani ya kuchangia fedha kwa ajili
ya ujenzi wa mabweni 30 ya wanafunzi wa kike.
Matembezi hayo
yataanzia katika eneo la Mlimani City kesho kuanzia saa moja hadi saa tano
asubihi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Uwekezaji na Uwezeshaji Mary Nagu. Akizungumza
na waandishi wa habari jana Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru
Kawambwa alisema kuwa matembezi hayo ni moja kati ya harakati ya kuchangisha
bilioni 2.3 kwa ajaili ya ujenzi wa mabweni hayo yatakayohudumia wanafunzi wa
kike 1,504.
Alisema kuwa
mikoa ambayo inahitaji mabweni hayo kwa wingi ni Mara, Kigoma, Rukwa, Tanga,
Dodoma,Manyara, Lindi na Magu .
Alisema kuwa
ni vema wananchi wakajitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za ujenzi wa mabweni
hayo kwa kununua fomu za ushiriki ambapo alisema kuwa fomu zinauzwa kwa
shilingi 20000/= katika ofisi za TEA.“ Mimi naona
kuwa hizi ni juhudi nzuri ambazo zinafanywa na hawa watu wa TEA kwa kushirikiana
na mabalozi wetu mbalimbali na kuna
jukumu la kila mmoja wetu katika kuhakikisha kuwa wanafunzi hawa wanasaidiwa
uhakika wao wa mahala pa kulala kwa kuwajengea hizi hosteli” alisema Waziri
Kawambwa.
Lengo la
serikali ni kujenga mabweni 100 kwa lengo la kuhudumia wanafunzi wa kike 4,800
nchini ili kuwanusuru na hatari ya kupata ujauzito wakiwa shuleni.






No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi