| Wakati mwagizaji nguli wa filamu nchini, Elizaberth Michael kwa jina la kisanii Lulu akisota rumande, kwa tuhuma za kumuua mwigizaji mwinzie Steven Kanumba, mwigizaji mwenzake Diana Kimaro,ambaye aliwahi kuigiza naye katika filamu ya Family Disaster akiwa kama dada yake wa karibu, na baadaye kufa kutokana na tabia ya kutembea na wanaume ovyo, ameamua kuokoka baada ya kuona hata yeye huenda akaingia matatizoni muda wowote. Mwigizaji huyo ambaye aliokoka katika kanisa la Chuo Cha Manabii lililopo Ubungo Maziwa July 29 mwaka huu, alisema ameamua kuokoka kwa sababu anasumbuliwa na roho chafu ambazo zilikuwa zikimwandama na kumyima raha. Aidha alisema msanii huyo ambaye aliingia kanisani hapo akiwa amevaa suluari nyepesi na T sheti ,amejifikiria sana na kuona anazidi kutanga tanga na ulimwengu, huku akiwa haudhulii katika nyumba yoyote ya ibada hali iliyomfanya aishi kwa mashaka. Hivi sasa amempokea Yesu kuwa bwana na mwokozi wa maisha yake na kuwa muumini wa kanisa hilo, ili kuepukana na mapepo wachafu |
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi