Wednesday, August 15, 2012

Ukimkamata mbanaji Cd za Bongo Movie MILIONI 2 CASH

                                   

Wasanii wa filamu leo kwa pmaoja walikutana katika viwanja vya Leaders Cloub kujadili juu ya hatma yao na maslahi yao katika tasnia hiyo na juu ya watu wanaobani Cd za filamu zao na kuuza kama njugu. Pia makundi mawili ambayo yalikuwa yakikizana siku zote kati ya kampuni inayojiita Bongo Movie chini ya mwenyekiti Jb na shirikisho la filamu nchini chini ya Saimon Mwakifamba, wamemaliza mgogoro wao huku kila mmoja akiweka ahadi kwa mwenzake kwamba anatambua uwepo wake. Miongoni mwa migogoro ambayo ilifanya mpasuka huo kuwa mkubwa pale Mwakifamba alipofika kwenye Tv fulani na kutangaza kwamba Bongo Movie haitambui kwa mujibu wa sheria,  huku akianika baadhi ya picha zinazoashiria kundi la Bongo Movie kwamba ndilo linaua tasnia kwa kufanya umalaya. lakini siku ya leo tofauti zote hizo waliziweka chini, na kuibua hoja mpya kwamba ni jinsi gani wanaweza kupambana na maharamia ambao wanadurufu kazi za wasanii na kuwafanya wawe mafukara daima. Miongoni mwa matukio ambayo walikubaliana kuyafanya ni kufanya maandamano makubwa yakiongozwa kwa kuvaa Tisheti, za kuashiri kupamba na uadui huo wa kudurufu kazi za wasnii. Huku wasnii mbalimbali wakitoa dau ili kukamilisha maandamano hayo, miongoni mwa watu waliotoa michango yao ni  Cloud 112 alitoa shilingi elfu 50, na usafiri wa kuelekea kwenye maandamano, Jb altoa laki moja, Tues Kinagala alitoa shiling laki moja na mengine wakasema watajua na kampuni yake cha kufanya, Dk Cheni alisema yeye atatoa usafiri, wakati wakubwa wao na wasambazaji wakubwa hapa nchini STEPS ENTERTAIMENT wakitoa ofa kwamba yoyote atayefanikisha kupatikana kwa mwaharamia mmoja basi atachukua donge nono la MILIONO MBIL . Kazi hiyo vijana wa mjiniii


Best naso na Mkwabi wa 69 Record

Wasanii wa kike walikuwa bize na magazeti
Mkono wa baraka wa heri, kati ya Jacob Stephan wa Bongo Movie na Saimon Mwakifamba wa TAFU
Libert ndani ya nyumba
Chopa wa Mchopanga akiwa na Mr Kupa
Mtitu akiwa na mdau wake

JB akitoa maneno yake
Mwakifamba akiikubali Bongo Movie kisheria
Hata hivyo tulipata muda wa kumkumbuka gwiji la filamu nchini, Steven Kanumba... Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi... Amin


Mahela yakihesabiwa


Irene Uwoya siku hizi ni mwendo wa kininja.


Uwoya na Odama
Sajuki na Dino
Kambarage na Jb wakiwa kwenye pozi
Jimmy Mafufu na Mtitu

M 2 ndani na yeye alikuwepo

Mzee wa Bongo Unit akiwa na Gelard wa Globar Publishers, Sam wa Ukweli na Mboto.

Mc alikuwa mama wa wasanii, Natasha

Sam wa Ukweli akiwa mbele ya Gari lake

Kiongozi wa STEPS
Richie Rich

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi