| Wakati mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ukiendelea, msanii Vicent Kigosi kutoka kampuni ya Rj anatarajia kuachia filamu yake ya Glory Ramadhan akishirikiana na Abdallah Khamisi 'Mwana Ambua'. Hakika si filamu filamu ya kukosa,kwani inaelezea juu ya maisha ya familia ya watu wawili ambao ni ndugu na kujifanya waislamu wazuri kumbe ni balaa tupu. Ray yeye mkewe ni Batuli, anajifanya mswahilina na kwenda kuswali tarawei,kumbe anaishi gest kinachokuja kumkuta ndipo utamu ulipo, wakati ndugu yake wa karibu Abdallah yeye mrevi kufuru wakati mkewe Chuchu Hansy ni mswahilina na anajaribu kumrudisha mumewe kwenye maadili. Lakini mwisho wa siku naye kilichompata, kinamfanya kunyooka bila ya kunyooshwa. |
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi